Monday, October 2, 2017

ALEX MSAMA AMPONGEZA WAZIRI HARISSON MWAKYEMBE KWA KUPIGA VITA WIZI WA KAZI ZA WASANII

01
Mkurugenzi wa Kampuni Msama Auction Mart , Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Kampuni hiyo Kinondoni Moroco jama wakati akipmogeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa hatua mbalimbali anazochukua kulinda kazi za wasanii zisiibiwa.
1
2
Mkurugenzi wa Kampuni Msama Auction Mart , Alex Msama akifafania jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumza nao.
3
Baadhi ya wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii  wakichukua matukio katika mkutano huo.
………………………………………………………………………….
Kampuni ya Msama Auction Mart imempongeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kauli yake kuhusu wizi wa kazi za sanaa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama amesema kuwa Kampuni yao imeona kuwa Waziri huyo ameonesha nia yakupoteza kabisa kazi feki za Sanaa.

Hatua hiyo ya Waziri pia itawagusa wenye kazi zao ambao ni Wasanii wa kazi hizo ikiwemo Wasanii wa Bongo Fleva, Nyimbo za Injili, Maigizo na Filamu.

Msama amesema kuwa doria za kumaliza wizi huo wa kazi za Wasanii inaendelea kwa nchi nzima, ambapo Mkoa mmoja tu ndiyo wenye ahueni yakupunguza wizi huo ambao ni Mwanza.

“Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inategemea kuanza zoezi lakumaliza kazi feki za sanaa nchini, zoezi ambalo lisilokuwa na mwisho”, amesema Msama.

Pia Msama ameonya wale wote wanaofanya biashara za kuuza kazi feki, ambapo amesema kuwa watakapokamata Kompyuta za kufanyia kazi hizo basi hazitarudi tena kwa wahusika.

Wafanyabiashara wa Filamu za Nje nao wametakiwa kuacha kufanya biashara hizo bila kibali cha mwenye kazi husika, kwani hatua hiyo inaikosesha Serikali mapato.

No comments:

Post a Comment