Wednesday, October 18, 2017

Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Aahidi kutatua kero Zinazowakabili Wamiliki Wa Shule Binafsi

Afisa elimu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na washiriki wa mkutano  uliowakutanisha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule binafsi (TAMONGSCO), Charles Totela Akizungumza 
Miongoni mwa wamiliki wa shule binafsi pamoja na wawakilishi waliofika kwenye mkutano  huo 

Na Michael Utouh
 
AFISA  Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis  Lissu  ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsiinafsi wa mkoa huo ikiwemo ya  tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule hizo .
 
Pia amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa kuwa wana walimu wengi wa masomo hayo.
 
Ameyasema hayo  leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu uliowakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa shule zilizopo mkoani humo.
 
Amesema wamiliki wa shule hizo pamoja na shule zao wanapaswa watambaue huduma wanazopewa  ni stahiki  hivyo ni sawa wanazopatiwa shule za Serikali.
 
“Natamani kuziona shule zote binafsi zikiwa zinazoongoza kutokuwa na changamaoto zozote kwani tunatambua mchango wa uwekezaji hapa nchini,” amesema.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini (TAMONGSCO), Charles Totela ameishukuru Serikali ya mkoa huo kwani imekuwa ikiwapa ushirikiano wa kutosha.
 
Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali ya mkoa huo kuwaundia dawati la pamoja litakalowakutanisha viongozi wote wa shule binafsi, za serikali na watendaji wao ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi.
 
Naye Mkurugenzi wa Shule za Al-Muntazir,  Mahmood Ladack amewashukuru wamiliki wa shule hizo kwa kuhitisha mkuatano huo ambao anataraji utakuwa na manufaa makubwa kwao na taasisi wanazosimamia katika kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment