Wanasiasa wa upinzani nchini Uganda Muhammad Nsereko na Allan Sewanyana
Mvutano mwingine unatarajiwa kushuhudiwa tena katika bunge la Uganda
wakati wabunge wa chama tawala NRM, watakapojaribu kuwasilisha ombi la
kuandaa mswada wa kubadilisha Katiba ya nchi hiyo.
Wabunge wa NRM wanataka kubadilishwa kwa
kifungu cha katiba cha 102, ibara ya b, ili kuondoa kikomo cha umri wa
mgombea urais nchini humo.
Hatua hii inakuja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021, ikitarajiwa kuwa iwapo mabadiliko hayo yatafanyika, rais Yoweri Museveni atakayekuwa na umri wa miaka 76, atawania tena urais .
Katiba ya Uganda inaeleza kuwa, mtu
hawezi kuwania urais akiwa na umri wa miaka 75 na zaidi, kifungu ambacho
wabunge wa NRM wanataka kiondolewe.
Mchambuzi wa siasa Kenneth Lukwago akiwa
jijini Kampala, amekuwa akiiambia RFI Kiswahili kuwa chama cha NRM
kinaona kuwa hakuna mtu anayeweza kuwania urais mwaka 2021 kupitia chama
hicho.
Pamoja na hilo, chama cha NRM kinaona kuwa njia pekee ya kuendelea kuwa madarakani ni kwa rais Museveni kuwania tena urais.
Aidha, kuna wale wanaona kuwa rais
Museveni ameongeza vema kwa zaidi ya miaka 30 na kutoa mfano wa
kuimarika kwa hali ya usalama na amani hasa Kaskazini nchini humo na
hivyo anastahili kuendelea kuongoza.
Hata hivyo, wanasiasa wa upinzani
wakiongozwa na Kizza Besigye wameapa kutoruhusu mabadiliko hayo huku
wakisema hawataki katiba kubadilishwa.
Siku ya Jumnne, hali ya usalama uliimarishwa nje ya bunge la jiji la Kampala na hasa maeneo ya bunge kuelekea vikao vya bunge.
Maandamano ya kupinga mabadiliko hayo pia yanatarajiwa kushuhudiwa.
No comments:
Post a Comment