Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na Wananchi
wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (kulia) akimkabidhi
nahodha wa timu ya Qatajiring zawadi mbalimbali mara baada ya kuibuka
kidedea baada ya kuifunga timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei
Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge
wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.
Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (aliyevaa miwani) akikagua
timu za Qatajiring na timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei
Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge
wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia
fainali ya Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu kati ya timu za Qatajiring na
timu Zahanati iliyochezwa katika kiwanja cha Dongobesh.
Picha na Eleuteri Mangi,WHUSM, Mbulu
……………………..
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu
Halmashauri zote nchini zimetakiwa
kutenga maeneo ya michezo wakati wa kupanga mipango miji kwa matumizi
bora ya ardhi katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura
alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya Jimbo Cup inayodhaminiwa na
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei
Massay iliyochezwa katika eneo la kata ya Dongobesh Wilaya ya Mbulu
Mkoani wa Manyara.
“Natoa wito kwa Halmashauri zote
ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya Mbulu wakati wa kupanga matumizi
bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji mkumbuke kutenga maeneo ya
michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa mafunzo ya michezo na
utaalam” alisema Naibu Waziri Wambura.
Akikabidhi zawadi za washindi
katika mashindano hayo ambao ni timu ya Qatajiring kutoka kijiji cha
tumati ambao ni mshindi wa kwanza na timu ya Zahanati kutoka kijiji cha
Diomati mshindi wa pili, Naibu Waziri Wambura amewahimiza wachezaji na
wananchi kuthamini michezo kwa kuwa ni ajira, inaleta umoja na
mshikamano miongoni mwa jamii.
Dakika 90 za fainali hizo ziliisha
kwa timu zote kufungana bao 2-2 na hatimaye timu ya Qatajiring iliibuka
kidedea kwa ifunga timu ya Zahanati kwa penati 4-1.
Akionesha umuhimu na umahiri wa
wilaya ya Mbulu katika michezo, Naibu Waziri Wambura amesema wilaya hiyo
imekuwa kitovu cha wanamichezo bora hasa mchezo wa riadha ambao
wameiletea sifa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Wanamichezo hao ni pamoja na John
Stephen Akhwari nguli mchezo wa riadha aliyeweka historia ya kimataifa
aliyewahi kusema “Nchi yangu haikunituma kuanza mashindano, ilinituma
kumaliza mashindano”Filbert Bai na wanaridha wengine.
Aidha, Naibu Waziri Wambura
amewashauri waandaaji wa mashindano hayo washirikishe pia mchezo wa
netiboli ili kuwaendeleza watoto wa kike katika mchezo huo.
Kwa upande wake mdhamini wa
mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay amesema kuwa
alivutiwa kuanzisha mashindano hayo ili vijana wajihusishe na michezo na
kuboresha na kuendeleza afya zao na kuachana na masuala yanayoweza
kupoteza maisha yao na nguvu kazi ya taifa.
Mashindano hayo yalishirikisha
timu 24 kutoka Mbulu Vijijini tangu kuanzishwa kwa mwezi Julai mwaka huu
na kufikia kilele Septemba 25 ambapo fainali ilichezwa katika viwanja
vya Dongobesh na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali na mashabiki lukuki
kutoka maeneo yote ya halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment