Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo( wa pili kushoto) akiwasili katika viwanja
vya Nyerere Square Mjini Dodoma kuzindua Maadhimisho ya Siku ya Wazee
Duniani kwa kuzindua maonesho ya shughuli za wazee za ujasiriamali,
kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na
Watoto Bw. Julius Mbilinyi .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiangalia moja ya bidhaa zilizopo katika
mabanda ya maonesho ya shughuli za wazee za ujasiriamali katika viwanja
vya Nyerere Square Mjini Dodoma kabla ya kuzindua rasmi Maadhimisho ya
Siku ya Wazee Duniani.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee
Tanzania Mzee Sebastian Bulegi akitoa salamu za wazee kwa Mgeni rasmi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (hayupo Pichani)
wakati wa uzinduzi rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Bw. Julius Mbilinyi akitoa neno kwa
niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto
kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani uliofanyika
katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.
Christina Mdeme akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa Maadhimisho ya Siku
ya Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wazee katika viwanja vya
Nyerere Square Mjini Dodoma wakati akizindua Maadhimisho ya Siku ya
Wazee Duniani.
Baadhi ya wazee kutoka mikoa
mbalimbali Tanzania wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika
viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa Maadhimisho
ya Siku ya Wazee Duniani.
Kikundi cha Ngoma cha Lusombi
kutoka Ruvuma kikiburudisha kwenye uzunduzi wa Maadhimisho ya Siku ya
Wazee Duniani uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya
Kitaifa ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani
yanayofanyika kwa mwaka 2017 Mjini Dodoma kwa kauli mbiu isemayo
:“Kuelekea Uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango,Uzoefu na Ushiriki wa
Wazee kwa Maendeleo ya Taifa”
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
No comments:
Post a Comment