Mkazi
wa Misungwi, Kwilokeja Boniface (35) amemuua mkewe Shija Luchagula
(30), kwa kumnyonga kisha na yeye kujinyonga kwa kile kinachodaiwa wivu
wa mapenzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana Jumatatu kuwa
tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha Mwiligiligili wilayani
Misungwi.
Alisema
mwanaume alitoka shambani akakuta tairi nyingi za baiskeli kwenye
uwanja wa nyumba yake ndipo ukazuka ugomvi baina yao akimtuhumu mkewe
kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao hivyo alianza kumpiga kwa fimbo kisha
kumnyonga mpaka akafariki dunia.
Alisema baada ya kufanya hivyo na yeye alichukua jukumu la kujinyonga kwa kamba ili kukwepa mkono wa sheria.
“Kwa
sasa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na vifo hivyo na miili
ya marehemu tayari imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa ajili ya mazishi"
No comments:
Post a Comment