Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ndg John Lipesi Kayombo leo 09/09/2017 amekabidhiwa vitabu vya ziada na kiada vya masomo mbalimbali zaidi ya vitabu 450.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika shule ya Sekondari Mugabe iliyoko Kata ya Sinza Manispaa ya Ubungo Shule ambayo Mkurugenzi Kayombo ameichagua kupata vitabu hivyo.
Akipokea vitabu hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania Ndg Muhammad Shaban au Aluta D.
Mkurugenzi Kayombo amesema anafarijika kuona wadau na Asasi kama hii ya Wazalendo wanasaidia kupunguza au kuondoa kabisa Changamoto katika sekta ya Elimu hususani Manispaa ya Ubungo.
Kayombo amemwagiza Mwl Mkuu wa Shule ya Sekondari Mugabe na walimu wote kuhakikisha wanavitunza vitabu hivyo na kuwaongoza wanafunzi kuvitumia vitabu hivyo katika kuongeza ufaulu na Maarifa.
Pia Kayombo alipata wasaa wa kusikiliza kwa uchache changamoto katika shule hiyo alipoambiwa kunashida ya uzio papohapo akasema nitachukua sehemu ya fedha toka kwenye mshahara wangu na nitachangia Tofari 1000,na Mifuko ya Saruji 50.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Asasi ya Wazalendo akasema nami nitaendelea kusaidia shule hii kwa sasa niongeze tu nitachangia Tofari 200 pia naangalia uwezekano wa kuongeza "Shelves" katika Maktaba ya Shule ya Sekondari Mgabe.
Naye Kaimu afisa Elimu Sekondari Bi Neema wakati wa dhifa hiyo amesema tumepata Mkurugenzi Mzuri mwenye nia ya kuijenga Ubungo Mpya hivyo tumtumie vizuri.
Mwl. Mkuu wa Shule hiyo Bi Phoebe H. Kayumbo hakuwa nyuma kutoa shukrani kwa Mkurugenzi Kayombo pamoja na Asasi ya Wazalendo kwa msaada huo na kuomba waendelee kuwachangia maeneo mengine ili Mugabe isonge mbele kitaaluma na iwe ya kwanza kitaifa katika ufaulu
Mwisho Mkurugenzi Kayombo ameuagiza uongozi wa shule ya Mugabe kutumia wadau wa Elimu kutatua changamoto za kielimu yeye kikubwa anachohitaji apewe taarifa tu kabla ya Utekelezaji wa Jambo lolote shuleni.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment