Na Kudra Mawazo, Zanzibar
Makamo wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassain amesema kuwa uwepo wa kamisheni ya kiswahili hapa Zanzibar ni
moja ya heshima ilopata zanzibar kwakuwa ndio kitovu cha kiswahili barani Afrika.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la
kwanza la kiswahili la kimataifa ambalo linafanyika Zanzibar kwa siku tatu
katika hotel ya Golden Tulip iliyopo malindi unguja.
Kongamano hilo limeudhuliwa na viongozi mbali mbali
kutoka katika jumuiya ya afrika mashariki na nje ya ,jumuiya ya afrika
mashariki,ambapo samia alizindua mpango mkakati wa kamisheni hiyo wa miaka
mitano (2017-2022).
Samia amesema kuwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo
wapo tayari kutenga bajeti kwa lengo la kuendeleza kamisheni hiyo,kwakuwa
umuhimuwa kamisheni hiyo ni mkubwa kwa kukuza lugha ya kiswahili katika mataifa
ya afrika na duniani kote.
Alisema kuwa dira ya EAC 2050 inalenga kuongeza kasi
ya utengamano wa kikanda,ambao ni umoja wa forodha,soko la pamoja,sarafu moja
na ushirikiano wa kisiasa, na kuifanya kamosheni hiyo kufikia malengo
yaliyokusudiwa kwa kukitangaza kiswahili na kutoa fursa kwa mataifa yalio nje
ya kumuiya ya afrika mashariki kujifunza kiswahili na kuwa na tafsiri moja ya
maneno mapya ya kiswahili.
Alisema lunga ya kiswahili ni kiungo muhimu katika kufikia
malengo hayo ambayo itasaidia kujenga utambuzi na kubaini changamoto na fursa
zinazofungamana na maendeleo hayo.
Samia alisema kuwa tanzania ipo tayari kutoa walimua
wa kiswahili kwa taifa la sudan ya kusini kwa lengo la kufundisha kiswahili
katika nchi hiyo baada ya kutoa maombi ya kupatiwa walimu wa kswahili.
Sudani kusini ni nchi ya sita ambayo imejiunga na
jumuiya ya afrika mashariki mwaka 2016,taifa hilo ni taifa ambalo kiswahili ni
lunga mpya kwa wanachi wao.
Mapema kaimu mwenyekiti wa baraza la mawaziri la
umoja wa afrika mashariki balozi Dk Augustine Mahiga alisema kiswahili ni
miongoni mwa lunga Zinazokuwa kwa kasi duniani na kubainisha haja ya
kuiendeleza ili kutimiza lengo la kuwaunganisha wananchi wa ukanda wa afrika
mashariki.
No comments:
Post a Comment