Afisa Utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Maureen Mbolene akitoa maelekezo kwa washiriki wa washa hiyo.
Meneja
na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare,
Euphrasia Shayo (kulia) akiwasilisha mada yake juu ya madhara ya
kemikali za vipodozi na mkorogo kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.
Sehemu ya washiriki katika semina hiyo.
Sehemu
ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii
wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 wakifuatilia mada
anuai toka kwa wawasilishaji.
Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo akiuliza swali mara baada ya uwasilishaji.
…………………………….
MATUMIZI ya vipodozi vyenye
kemikali ya sumu yamewatisha wakulima katika Tamasha la Jinsia Tanzania
2017 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao, Mabibo jijini Dar es
Salaam.
Hofu hiyo ilitanda jana baada ya
Meneja na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare,
Euphrasia Shayo kuwasilisha mada yake kwa kundi hilo la wakulima
wanaoshiriki tamasha la jinsia kutoka maeneo anuai.
Alisema kemikali za sumu kama
zebaki na mericuri zilizomo katika vipodozi na mikorogo isiyo rasmi
inayotumiwa hasa na akinamama kujichubua na kubadili nyele zao zina
madhara makubwa katika kilimo.
Alisema kemikali hizo mbali na
kukaa ardhini kwa muda mrefu zaidi zikiharibu mazao pia vinamadhara
makubwa kwenye miili yao, hivyo kuwashauri kuachana navyo mara moja kwa
watumiaji.
Alisema kemikali hizo mara baada
ya kutumiwa hutelekezwa ardhini na mara mvua zinyeshapo husafirishwa
hadi katika vyanzo mbalimbali vya maji hivyo kujikuta vikitumiwa tena na
jamii jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya binadamu na mifugo.
“…Vinamadhara makubwa katika miili
yetu, ndio maana sasa hivi magonjwa ya ajabu ajabu ikiwemo kansa
vimeendelea kushamiri kwetu, vinginea husababishwa na kemikali hizi
zenye sumu. Wapo akinamama wameathiriwa vibaya sana na kemikali hizi
zenye sumu,” alisema Bi. Euphrasia Shayo.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima
wakishiriki katika mjadala waliiomba Serikali kuwatumia wataalamu kama
Bi. Euphrasia Shayo kutoa elimu ya madhara kwenye redio na luninga ili
kila mmoja aelewe madhara ya vipodozi hivyo.
Haya hivyo waliiomba kuendeleza
oparesheni la kuwakamata na kuwachukulia hatua kali waingizaji wa
vipodozi vyenye viambata vya sumu ili kupunguza madhara kwa jamii.
No comments:
Post a Comment