Mahakama
ya Hakimu ya Mkazi Kisutu, imepanga Oktoba 6, mwaka huu kutoa hukumu
katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Yusuf Manji(41).
Uamuzi
huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi , Cyprian Mkeha, baada ya
wakili wa utetezi Hajra Mungula kusema kuwa ameshafunga ushahidi wa
mashahidi saba.
Mashahidi
watatu wa upande wa mashtaka wametoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa
Daktari Mfawidhi wa Gereza la Keko, Inspekta Eliud Mwakawanga ameileza
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi maisha ya mfanyabiashara Yusufu
Manji yalivyo kuwa gerezani kwamba alikuwa akitumia vidonge kati ya 25
mpaka 30 kwasiku.
Ameeleza
kwamba walikuwa wakimpatia dawa hizo alipokuwa akisikia maumivu hasa
ya mgongo na kwamba kuna kipindi alikuwa anaamka akiwa na hali ya
kutetemeka au kuchanganyikiwa.
Ameeleza
kuwa Julai 6, 2017 walimpokea Manjia kitokea Hospitali ya Muhimbili
Kitengo cha Moyo cha JKCI ambapo waliambiwa ni mshtakiwa lakini ni
mgonjwa.
“Nilienda kumuona, tukazungumza naye na tulikaa naye gerezani hadi alipokuja kuachiwa,”
No comments:
Post a Comment