Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu pamoja na viongozi wengine wakifatilia taarifa ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi.
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya wachimbaji wadogo wadogo ya AMINIKA Ndg Hamisi A. Nkingi akisoma taarifa ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi hiyo kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Na Mathias Canal,
Singida
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekubali ombi la viongozi wa
Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA la kuwa mlezi wao Sambamba na
kuchangia Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kusaidia Kupunguza ukali wa
changamoto zinazowakabili.
Chama hicho Cha
USHIRIKA wa wachimbaji wadogo (AMINIKA GOLD MINE CO-OPERATIVE SOCIETY LTD)
chenye jumla ya wanachama 193 Ni muungano wa vikundi vitano vya Uchimbaji mdogo
wa Madini ya dhahabu vinavyotokana na vikundi vya Elimika-Sambaru,
Amka-Sambaru, Amani-Sambaru, Aminifu-Mang'onyi na Muungano-Mlumbi.
Akizungumza na
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya AMINIKA Mhe
Mtaturu alimuagiza Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha E. Msemo
kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu mwenendo wa Chama hicho.
Alisema kuwa
Uongozi wa Wilaya unatambua umuhimu wa Chama hicho kutokana na umahiri wake na
muelekeo wa kuwakomboa wachimbaji wadodo katika Wilaya ya Ikungi.
Alisema ili Chama
hicho kuwa na Ushirika mzuri na mafanikio makubwa Ni vyema viongozi
watakaochaguliwa kutanguliza maslahi ya wananchi mbele kwa kusoma taarifa kwa
uwazi na ukweli.
Mhe Mtaturu
alisema mafanikio ya Chama Cha Ushirika Cha AMINIKA Ni pamoja na kuchagua
viongozi Bora watakaokuwa na mikakati makini kea ajili ya kukikomboa Chama na
kuwa na mbinu zenye manufaa kwa ustawi wa Chama.
"Wapo watu
wanaodhani kuwa kuzaliwa kwenye eneo la Madini Basi inakufanya kuwa mtaalamu wa
Madini, nataka niwaeleze kuwa Madini yanataka utaalamu, mtaji na teknolojia
hivyo sisi Kama serikali tunawahakikishia kuwa tutashirikiana nanyi bega kwa
bega" Alisema Mtaturu
Aliongeza kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
anawathamini wachimbaji wadogo endapo watakuwa na mipango Bora ya maendeleo
katika uchimbaji.
Akizungumza kwa
niaba ya mwanachama menzake wa Chama hicho Cha Ushirika Cha wachimbaji wadogo
wadogo Bi Elizabeth Shango alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwa kukubali
ombi la kuwa mlezi wa Chama hicho Cha Ushirika ambapo alipongeza pia namna
ambavyo Dc Mtaturu Ameanza malezi ya Chama hicho kwa kuchangia Shilingi Milioni
Moja.
Uchaguzi wa
Viongozi wa Bodi ya Chama hicho Cha USHIRIKA Cha wachimbaji wadogo (AMINIKA
GOLD MINE CO-OPERATIVE SOCIETY LTD) kinafanya uchaguzi wa awamu ya Pili kwa
kipindi Cha miaka mitatu 2017/2020 mara Baada ya Uongozi uliopo madaraka
kumaliza muda wake kwa kipindi Cha awamu ya kwanza Mwaka 2014/2017.
MWISHO
No comments:
Post a Comment