Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwapa akina mama waliojifungua mabeseni kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa kinamama wa jimbo la mufindi na wananchi wote wanotumie hospitali ya mafinga mjini lakini mabeseni hayo yametolewa kwa msaada wa ubalozi wa kuwait hapa nchini Tanzania.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na mmoja wa kinamama alifanikiwa kupewa msaada wa beseni
Na Fredy Mgunda,Mafinga.
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mabeseni mia moja kwa akina mama waliopata watoto kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Mafinga.
Mabeseni hayo yalikabidhiwa kwa kina mama waliojifungua na ambao wanatarajia kujifungua hivi karibuni hospitalini hapo.
Msaada huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni nne, umetolewa na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini mapema wiki iliyopita.
`ndugu zangu zawadi hii tumepewa na Balozi wa Kuwait hapa Nchini kwa ajili yenu kina mama kama sehemu ya mwanzo wa ushirikiano kati ya Mafinga na Ubalozi wa Kuwait' alisema Chumi.
Akifafanua, alisema kuwa msaada huo ni uthibitisho wa upendo alionao Balozi wa Kuwait hapa nchini kwa watu wa Mafinga.
`Mheshimiwa Balozi Jasem Al- Najem hajawai kufika Mafinga lakini kwa upendo mkubwa akasema, naomba hiki kidogo uwafikushie kina mama wa Mafinga' alisema Chumi na kuongeza kuwa ushirikiano kwenye jambo dogo ndio mwanzo wa ushirikiano wa mambo mengine makubwa.
Akishukuru wakati wa kukabidhi msaada huo wa mabeseni, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga alipongeza ushirikiano wa Mbunge na wadau mbali mbali na kuwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma.
`sisi halmashauri tuko bega kwa bega na mbunge, na ninyi watumishi kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kujituma' alisisitiza Makoga.
Wakati akikabidhi msaada huo wiki moja iliyopita kwenye ofisi za Ubalozi wa Kuwait Masaki Jijini Dar es Salaam, Balozi Jasem Al-Najem alisema kuwa lengo la Ubalozi ni kugawa jumla ya mabeseni elfu moja kwa ajili ya mama na mtoto.
`katika awamu ya kwanza ya kutoa msaada huu wa mabeseni haya ya mama mtoto kits, tumeona tuwakumbuke na kina mama wa Mafinga japo kwa mabeseni mia moja'
Ubalozi wa Kuwait umekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii na kibinadamu ambapo mpaka sasa wameshachimba visima arobaini kwenye shule mbali mbali za Mkoa wa Dar na Pwani.
Aidha Ubalozi umeshatoa msaada wa vifaa vya theatre katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na pia kuendesha zoezi la kuchangia damu miezi sita iliyopita.
No comments:
Post a Comment