FAMILIA 13 zenye watu 44
zimeathiriwa kwa moto ulioibuka kwenye nyumba wanazoishi askari polisi
katika Kata ya Sekei mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo ambaye pia aliwahi kufika eneo la tukio usiku huo amesema taarifa
za awali zinasema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme na uchunguzi
unaendelea. Gambo amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Andrew Komba amesema moto huo umeshadhibitiwa. “Tungefika mapema nusu ya nyumba zilizoteketea tungeziokoa,” amesema Komba.
Amesema taarifa kuhusu tukio hilo
zimewafikia kwa kuchelewa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles
Mkumbo amesema hali ni shwari na hakuna wizi uliotokea. Amesema tukio
hilo ni janga, hivyo watakaa kuona ni kwa namna gani watawasaidia
walioathiriwa.
No comments:
Post a Comment