Saturday, September 30, 2017

90% yaa Bajeti ya Afya Kinondoni inatumika kutibu magonjwa yanayotokana na Uchafu

Mstahiki meya wa Halmashauri ya Kinondoni Jijini Dar es salaam Benjamini Sitta, amewaeleza wannchi wa kata ya kawe kuwa asilimia  90 ya bajeti ya Afya katika Halmashauri hiyo inatumika kutibu mgonjwa yanayosababishwa na uchafu.
Ameyasema hayo mbele ya wakazi wa kata ya kawe Ukwamani leo katika Ijumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi ambapo amweataka wakazi hao kutunza mazingira ili kuepusha mlipuko wa magonjwa na kwamba kufanya hivyo itachochea maendeleo ya kata hiyo kwakuwa nguvu kazi itakuwa na afya njema

 Hata hivyo katika kero ya ujenzi wa daraja la Ukwamani Mstahiki meya ameahidi kuanza mara moja tathmini ya ujenzi wa daraja hilo ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza madhara ambayo yamekuwa yakitokea hasa nyakati za masika.
Hata hivyo amewahimiza wananchi hao kujitoa kwa hali na mali ili kuchochea kwa kasi maendeleo ya kata hiyo ili kuendana kasi ya serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake Diwani wa kata kawe Muta Lwakatare  amemueleza mstahiki meya kuwa kero kubwa katika eneo hilo ni daraja la ukwamani ambalo limekata mawasiliano ya pande mbili za kata hiyo, ambapo amemuhakikishia ujenzi wa daraja hilo maramoja ili kuendana na kasi ya maendeleo kwenye kata hiyo.

Mbali na hayo wananchi hao wameelezwa kuwa Manispaa imetengwa kiasi cha shilingi bilioni 2 kwaajili ya mikopo ya akina Mama na vijana wajasiriamali kwamba wahakikishe wanakopa na kurejesha ili wanufaike kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment