Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua daraja lililopo kwenye barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wakiwa na Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wakati wa ziara ya Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Watani kwa Jongo katika Kata ya Makurumla. Leo Agosti 14
Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakimsikiliza kwa makini Mtaalamu wa Barabara akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Kifuru-Msigani wakati wa ziara ya kukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
Muonekano wa Barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa katika hatua za awali za ujenzi.Leo Agosti 14
Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo wamefanya ziara katika miradi ya barabara
inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa lengo la kujua
Maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni Barabara ya Watani kwa Jongo Kata
ya Makurumla ambayo ina Urefu wa kilomita 1 na inajengwa kwa kiwango cha
changarawe kwa kutumia fedha za Ndani (own source), Barabara ya Ubungo Msewe
kutokea Kimara Baruti yenye urefu wa
Kilomita 2.6 inasimamiwa na TAN ROADS, Pia Barabara ya Kifuru – Msigani yenye
urefu wa kilomita 4.0 ambayo ina simamiwa na TAN ROAD na inajengwa kwa kiwango
cha lami.
Wajumbe wa bodi ya Barabara hiyo wamedhamiria kuhakikisha
miradi iliyopangwa inatekelezwa kwa
wakati na kwa ubora ili kuboresha miundo mbinu ambayo itawanufaisha na
kuwaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Wajumbe hao kwa Upande wa Manispaa ya Ubungo ni Mhe. Mbunge
wa viti maalumu Suzan Lymo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi
Kayombo, Katibu tawala wa Wilaya Ndg James
Mkumbo na Wataalamu kutoka ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment