Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka
akizungumza katika Mkutano wa ndani wa Wanachama na Viongozi wa CCM na
Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin pemba.(Picha Zote na Fahad Siraji)
Kaimu
katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na
viongozi wa chama mkoa wa kaskazini unguja akiwa katika ziara ya
kikazi visiwani pemba.
Kaimu
katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akipokelewa na
viongozi ofisi za CCM wilaya ya micheweni katika ziara ya kikazi
visiwani pemba.
Vijana
wakiburudisha kwa kupiga dufu wakati wa mapokezi ya Kaimu katibu mkuu
wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shakaalipowasili ofisi za CCM
wilaya ya micheweni katika ziara ya kikazi visiwani pemba.
Kaimu
katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia
pamoja na mkuu wa idara ya Uchumi uwezeshwaji na fedha (UVCCM)Dorice
Obedi wakisain Vitabu vya wageni walipowasili wasili katika ofisi za CCM
Wilaya ya micheweni ziara ya kikazi visiwani pemba.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka
akizungumza jambo pamoja na mwl,Ally khatibu Hassan Mkuu wa shule ya
msingi Michekweni wakati akikagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na
madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni. wakati wa ziara ya kikazi
visiwani pemba.
Wanafunzi
wa Darasa la kwanza Issa Haji (wa kwanza kulia) pamoja na Abdulwahid
abdallah wakisalimiana na Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM
Shaka Hamdu Shaka wakati alipokwenda kukagua jengo la Ujenzi wa
maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akimfunga
Vifungo vya shati Mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi
Micheweni Abdulwahid abdallah wakati alipokwenda kukagua jengo la
Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni.
Kaimu
katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akigagua ujenzi
wa ofisi ya ccm tawi la njuguni inayojengwa na mwakilishi Jimbo
Afisa
mipango wa halmashauri ya konde (pili kushoto)akitolea ufafanuzi juu ya
ujenzi wa soko la mboga mboga la samaki pamoja na mbogamboga kwa Kaimu
katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa katika
ziara ya kikazi visiwani pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM
na Jumuiya zake Tawi la kuiyu Mbuyuni akiwa katika Ziara ya Kikazi Mkoa
wa Kaskazini pemba .
Wanachama Wa CCM na Jumuiya zake wakishangilia katika mkutano wa ndani uliofanyika Skuli ya Michekweni.Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ustadh,Abdul mohammed akifungua kwa Kusoma quran Tukufu katika ukumbi wa Skuli ya Michekweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha (UVCCM) ndg:Dorice Obed
akizungumza katika Mkutano wa ndani wa Wanachama na Viongozi wa CCM na
Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin pemba.
Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni wakifuatilia kwa Umakini mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha ndg:Dorice Obed akicheza nyimbo ya CCM pamoja na wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin Pemba
Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha ndg:Dorice Obed akicheza nyimbo ya CCM pamoja na wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin Pemba
Na
Mathias Canal, Kaskazini Pemba
Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa Jukumu la kuleta maendeleo ya kiuchumi
katika jamii ni la kila mwananchi sio jukumu la serikali pekee.
UVCCM imesema kuwa
jukumu la serikali ni kuwaonyesha wananchi fursa zilipo na namna bora ya
kuzichanganua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ili kukuza uchumi wa mtu mmoja
mmoja na jamii kwa ujumla wake sambamba na kuwezeshwa kupata mikopo katika
vikundi vyao vya ujasiriamali.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka
Hamdu Shaka leo Agosti 16, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa
Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kuwa vijana ni
nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kutumia nguvu zao vizuri kwa kufanya kazi
ili kujikwamua kiuchumi katika familia zao badala ya kukaa maskani kujadili
mambo yasiyokuwa na tija kwao.
Aliongeza kuwa UVCCM
inaunga mkono vijana kukaa maskani kwa maslahi mapana ya mjadala wa Maendeleo
yatakayopelekea kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi
mbalimbali vya ujasiriamali.
Shaka alisema kuwa Kila mwananchi kwa nafasi yake anatakiwa
kuwajibika kwa nafasi aliyonayo ndani ya chama ama serikali kwani wananchi
wanataka maendeleo ya uchumi wao sio ahadi hewa za majukwaani.
Aidha, alisema kuwa Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt John Pombe Magufuli ipo pamoja na watanzania wote ambao ni wanachama wa
Chama Cha Mapinduzi ama wale ambao sio wanachama wa vyama vya siasa kwani
mchakato wa maendeleo hauangalii itikadi za vyama vya siasa.
Alisema wananchi
wanatakiwa kutumia Tunu ya amani, umoja na mshikamano uliopo nchini kufanya
shughuli za maendeleo na kujiepusha na maneno ambayo yataleta chokochoko za
kuondoa mshikamano katika jamii.
Shaka alisema kuwa vijana
wanatakiwa kujiajiri katika ujasiriamali kwa kuchukua hatua za makusudi za
kujiajiri kwani kusubiri ajira za serikali zitawachelewesha na pengine kufikia
hatua ya uzee pasina kuajiriwa kutokana na uchache wa ajira serikalini na wingi
wa vijana.
Kaimu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Vijana UVCCM ameanza ziara ya kikazi jana Agosti 15, 2017 visiwani
Pemba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi
ya mwaka 2015-2020.
MWISHO
No comments:
Post a Comment