Na: Pasco Nkololo
Huenda ikawa sio ajabu tena leo kusikia DRC Congo ipo nafasi ya 44 katika viwango vya ubora wa soka duniani wakati huo Tanzania ipo nafasi ya 114.
Hatushangai tena kwa kuwa tumeshaizoea hali, tumeipokea na kuridhika na kuhisi ndio nafasi yetu, hatuna bahati labda n.k
Licha ya mapenzi yetu katika mchezo huu wa soka lakini bado tumeonekana kutokua na bahati nao kamwe.
Leo tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa shirikisho lenye dhamana na mchezo wetu pendwa-TFF siku ya jumamosi pale Dodoma katika ukumbi wa St Gasper nadhan inapaswa kuwa wakati sahihi wa kujitazama na kujisahihisha ili iwe kama *turning point* kuelekea matarajio na matamanio yetu kwenye mchezo huu
Mpira wa dunia ya kisasa umebadilika mno, unahitaji akili kubwa, weledi na uwezo wa hali ya juu kuanzia kwa wadau ndani na nje ya uwanja,.
Mpira ni biashara, mpira ni ajira, mpira ni chanzo cha kuaminika cha mapato na ukombozi wa familia na kaya nyingi za kimaskini.
Na ni katika maono hayo ndipo unapoona uhitaji wa watu makini, wenye sera na maono kuelekea matarajio mapya ya soka letu
Tunapoenda kufanya uchaguzi wa viongozi wetu ni wakati sasa wa kuchagua si tu viongozi bali viongozi wa kutuvusha kutoka hapa tulipo.
Taifa lenye wakazi million 50 kukosa team ya wachezaji 25 wa kuunda team ya taifa na kuitoa nafasi ya 114 ni matokeo ya kukosa watu wenye maono ya soka katika mifumo yetu ya soka.
Na ni hapa ndipo tena naiona nafasi ya FREDEICK MWAKALEBELA kama mdau mwenye sera zenye uelekeo wa mabadiliko na mapinduzi kuelekea soka la kisasa.
The guy ni smart ana maono na uzoefu wa muda mrefu katika kada hii nadhani anatufaa sana na anaweza kutuvusha.
Twendeni na Mwakalebela
No comments:
Post a Comment