Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
Ndg Shaka Hamdu Shaka akipanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya kutunza
Mazingira wakati wa ziara yake katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa
Kusini Pemba
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwasili katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa
Kusini Pemba kwa ajili ya kujionea hali ya upandaji miti aina ya Mikoko
unavyoendelea.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo na Mdhamini wa Shirika la Bodi ya Taifa
ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya
ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa
ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Zao la
Karafuu likiwa limehifadhiwa ghalani chini ya Shirika la Bodi ya Taifa ya
Biashara Zanzibar
Vijana wakijishughulisha na shughuli za ubabeji mizigo katika
ghala la kuhifadhia zao la Karafuu, Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza maelezo mbalimbali ya Mdhamini wa Shirika la
Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea
hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba
wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Na Mathias Canal, Pemba
Zanzibar ni
maarufu kwa uzalishaji wa karafuu ulimwenguni kwa zaidi ya karne mbili
sasa. Uzalishaji huo ulikuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia tani
35,000 mwaka 1830 na kumiliki soko la karafuu duniani kwa asilimia 90.
Iliongoza
katika uzalishaji wa zao hilo kuanzia mwaka 1830 hadi 1940 kabla ya nafasi hiyo
kuchukuliwa na Indonesia.Tathmini iliyofanywa hivi karibuni ya Sensa ya Miti
(Woody Biomass Survey 2013) imeonesha kwamba Zanzibar kwa sasa ina idadi ya
mikarafuu 4,131,783, ambapo Unguja pekee ina zaidi ya mikarafuu 277,196 na
Pemba zaidi ya mikarafuu 3,854,587.
Tathmini ya
mwaka 1997 ilionesha idadi ya mikarafuu 790,400 kwa Unguja na mikarafuu
5,042,700 kwa upande wa Pemba, ikifanya idadi ya mikarafuu yote kuwa ni
5,833,100
Kaimu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amelitaja zao la karafuu kuwa ni
zao muhimu kwa uchumi wa taifa ambalo huongeza kwa kiasi kikubwa kipato kwa
wananchi.
Alisema
katika kuimarisha zao la karafuu Zanzibar, pamoja na kupambana na mabadiliko ya
tabia ya nchi kuna haja ya kupandwa mikarafuu na minazi maskulini, ili wanafunzi
waweze kupata uwelewa zaidi wa kutunza na kulienzi zao hilo, kwa maslahi yao na
taifa kwa ujumla.
Shaka
alisema hayo wakati alipotembelea na kupanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya
kutunza Mazingira ili kuhuisha uoto wa asili na kuepuka mmomonyoko wa ardhi
katika eneo la Mwambe lenye asili ya Watumbatu Wilaya ya Mkoani na Mkoa Ni
Kusini PEMBA.
Pia
aliwasisitiza wananchi kuhusu kupanda miche ya mikarafuu na minazi na kutotupa
taka ovyo ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi.
Alisema kuwa
serikali inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa inaandaa sheria kali itakayokuwa
maalumu kwa kuwachukulia hatua wananchi wanaokata miti ovyo kinyume na
utaratibu.
Katika hatua
nyingine Shaka alitembelea shirika la Taifa la Biashara Zanzibar kujionea hali
ya ununuzi wa zao la karafuu ambapo alimpongeza Mdhamini wa wa shirika hilo Ndg
Seif Suleiman Kassim kutokana na kiwango kikubwa cha ukusanyaji wa zao hilo
ambapo katika msimu huu hadi kufikia Mwezi Julai 13, 2017 tayari 2203 sawa na
Kilogramu 99180.0 zilikuwa zimehifadhiwa kwa ajili ya kupelekwa Unguja.
Alisema
uzalishaji wa zao la karafuu, katika Wilaya ya Mkoani unaongoza kwa zaidi ya
asilimia 60 ya uzalishaji wa zao hilo kwa zanzibar, na amewataka wananchi
kuendelea kutunza mikarafuu, kwani ndio pato la Taifa.
Zanzibar ni
visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika miaka 30 ya
nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani 8,605
zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka.
Jamii ya
wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana karafuu
ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza vituoni
tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza.
MWISHO
No comments:
Post a Comment