Sehemu ya kauli zilizotamkwa na Kaimu Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza ofisini kwake mjini Iringa alipokutana nae kufanya mazungumzo ya kuimarisha mahusiano baina ya UVCCM na Serikali ya Mkoa leo 10/08/2017
*Dhamira njema ya UVCCM kukifufua chuo hiki ni kuendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali ya awamu ya Tano na kifikra na Falsafaza katika uchumi wa viwanda , Uadilifu, ushapakazi, uzalendo na ujasiriamali za Mwenyekiti wa CCM Mhe. Dr. John Pombe Magufuli.
*Hakuna taifa lolote lile Duniani lenye uwezo wa kuwapatia vijana wote Ajira,Tumedhamiria kukifufua chuo hiki ili vijana wenzetu tuwapike na kuwafundisha stadi za maisha, ujasiriamali, ufundi, uzalendo, siasa na Itikadi ya chama chetu.
*Hii itawawezesha vijana kuendesha miradi yao kwa ufanisi zaidi.
*UVCCM imedhamiria kwa dhati kuwapika na kuwaoka vijana katika fani za uongozi na maadili na uzalendo kwa Taifa na kwa chama cha Mapinduzi.
*Fursa hii itawawezesha vijana kuandaliwa kisaikolojia, kujitegemea na kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kwa uadilifu wa hali ya juu.
*UVCCM imeona njia pekee ya kumuunga mkono Mhe Rais. Dk. John Pombe Magufuli ni kuinua maisha ya vijana dhidi ya umasikini na matumizi bora ya rasilimali za taifa.
*Nguvu kazi ya Taifa ni vijana wenyewe kujitambua, kujituma na
kujitegemea kisera, mipango chini ya programu nzuri za serikali ya awamu ya tano za kutaka kurudisha uzalendo, ufanisi kiuchumi, kisiasa na Kijamii pamoja na Fikra sahihi na chanya za kizalendo za Muasisi wa Taifa Letu Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K. Nyerere zimetusukuma UVCCM kufikiri upya umuhimu na ulazima wa kukifufua chuo hiki cha mafunzo kwa namna bora na endelevu ili kukifanya kiwe kituo Rasmi kitakachotumika kuwapika na kuwaandaa vijana wa CCM kupitia mafunzo ya itikadi, maadili, Uzalendo na Uchapakazi utakaosaidia kuinua na kustawisha Tanzania Mpya na CCM Mpya kwa kipindi cha sasa na baadaye.
Mapema Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka alitembelea na kukagua hatua za mwisho za maandalizi ya marekebisho ya chuo cha UVCCM Ihemi Iringa ambacho kinatarajiwa kuanza tena kutoa mafunzo kwa vijana mapema mwezi Septemba mwaka huu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment