Na Tiganya Vincent- RS-TABORA
SERIKALI
imewaonya wanafunzi kuepuka matumizi ya dawa za kulevya ambayo ndio
wakati mwingine yawasababisha kujiingiza vya uhalifu na vurugu ambazo
hatimaye zinawasababisha baadhi yao kusimamishwa masomo na kukatiza
ndoto zao.
Agizo
limetolewa jana wilayani Tabora na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya wakati alipotembelea
Shule ya Sekondari ya Tabora ili kujionea maendeleo ya ukarabati chini
ya utaratibu wa ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini.
Aliwaambia
kuwa wanafunzi wote nchini wanatakiwa kufuata Sheria za Shule na za
Nchi ili kuhakikisha anamaliza masomo yake bila kupata matatizo ikiwemo
kufikishwa mahakamani.
“Unatakiwa
kufuata Sheria na taratibu za shule kama ulivyoelekeza , ukitoroka
shule na kwenda mitaani ukileta fujo …ukileta vurugu utashughulikiwa
kama ulivyokutwa huko huko…kwa sababu mwanafunzi anatakiwa kuwa eneo la
shule sawa “ alisisitiza Naibu Waziri huyo.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri huyo aliwataka Wanafunzi wa Shule za
Wasichana ya Tabora kuepuka kujiingiza katika vitendo vitakavyokatisha
ndoto zao kwa sababu ya kupata ujauzito.
Alisema
kuwa vema kwa wakasoma kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza
kukatisha ndoto zao kwani jamii na taifa linawategemea sana kuja kushika
nafasi mbalimbali.
Naibu
Waziri huyo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wawe tayari
kukabiliana na ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Aidha
Manyanya aliwataka walimu wanaofundisha shule za watoto wenye vipaji
maalumu kuhakikisha wanajituma kwa bidii katika kuwafundishi wanafunzi
hao ili waendelee kufanya vizuri kama walivyotoka shule za awali.
Alisema
kuwa itasikitisha sana kuona mtoto aliingia katika shule hiyo kwa ajili
ya kipaji chake maalumu na inapifika mitahani yake anashindwa au
anafanya vibaya kinyume na ilivyokuwa hapa awali.
Akitoa
taarifa ya ukarabati unaoendelea Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tabora
Marwa Robert alisema kuwa hadi hivi sasa kazi mbalimbali ukarabati
unaendelea vizuri na zimebaki siku 60 ili mjenzi akabidhi kazi.
Alisema
kuwa ukarabati huo utagharimu shilingi milioni 999 ambapo hadi hivi
sasa kazi zilizokwishafanyika ni pamoja na kubomoa na kuziba nyufa,
kupaka rangi, ukarabati wa madirisha , milango, kurejesha vyoo,
ukarabati wa maktaba ya zamani, ujenzi wa maktaba mpya na kuandaa miundo
mbinu ya maji.
Hivi
karibuni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Milambo walitoroka shuleni
usiku na kuvamia sherehe za mkazi wa Tabora na kusababisha hasara kubwa
na kujeruhi baadhi ya watu.
No comments:
Post a Comment