Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amempiga biti Mbunge na viongozi wa upinzani mkoani Tanga kutojisifia
kuwa wao wameleta mradi wa Bomba la Mafuta katika eneo la Chongoleani
Tanga.
Rais
Magufuli amesema kuwa asitokee mtu yoyote katika jimbo hilo na kusema
kuwa mradi huo wa bomba la mafuta ameuleta kwani mradi huo umeletwa na
serikali ya Magufuli chini ya Chama Cha Mapinduzi.
"Hili
bomba la mafuta lingeweza kwenda kokote hapa Tanga, tungeweza
kulipeleka hata katika majimbo mengine ambayo yapo chini ya CCM lakini
tumelileta hapa Chongoleani, sijui hata chama gani kwa sababu serikali
yangu haibagui chama inataka kuleta maendeleo ya wananchi, hivyo
tumeleta hili bomba la mafuta hapa ili kuleta maendeleo kwa wananchi
asitokee mtu yeyote akasema amelileta hili bomba, ashindwe na alegee,
limeletwa na serikali ya Magufuli" alisema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli na Rais wa Uganda Museveni leo tarehe 5 Agosti 2017
wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima,
Kaskazini mwa Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Kata
ya Chongoleani Tanga ipo katika Halmashauri ya Tanga Mjini, jimbo
ambalo lipo chini ya Mbunge Mussa Mbaruk kwa tiketi ya Chama Cha
Wananchi (CUF)
No comments:
Post a Comment