Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango
kwa zawadi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya
Wilaya ya Nachingwea kabla ya kufunga maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika
viwanja
vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.
Na Mathias Canal, Lindi
Halmashauri
ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imeshika nafasi ya tatu katika
maonyesho ya nane nane ambayo huhusisha maswala ya Kilimo Mifugo na Uvuvi yaliyofanyikia Jijini Mbeya kwa kanda ya kusini na kuhudhuliwa na
viongozi mbali mbali.
Akizungumza
mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo
ya nanenane Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango aliwapongeza
wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho
hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Wila ya Nachingwea sekta ya Kilimo inasaidia
kuinua kipato kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Mimi
niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya
ya Nachingwea maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote
za kanda ya kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali
na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu" Alisema Muwango
Muwango alisema kuwa atakaa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea
Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza
na kuwa wilaya ya mfano.
Aidha, Muwango alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.
"Mikakati
iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho
mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na
ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie
ushindi mnono zaidi" alisema Muwango
Katika Maonesho hayo nafasi ya pili imechukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi huku nafasi ya kwanza ikinyakwa na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Katika maadhimisho hayo ya Nanenane 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan alisisitiza zaidi wananchi katika mkoa wa Lindi na Mtwara kutumia pesa walizopata wakati wa mavuno kujenga makazi bora,
kusomesha watoto na kununua chakula cha kutosha familia zao.
Aidha
aliwasifia wakulima hao kwa namna ambavyo wameweza kupokea teknolojia
za kilimo hivyo kubadilisha sura ya maonesho ikilinganishwa na maonesho
ya mwaka jana.
MWISHO
No comments:
Post a Comment