Thursday, August 10, 2017

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 1 WILAYANI BUKOMBE

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga ,na Kiongozi Mkuu wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kwenye Kijiji cha Nampalahala.

Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga baada ya kukabidhiana mbio za mwenge .


Kiongozi wa Mbio za Mwenge akiwa amebeba mwenge wa uhuru kwaajili ya kukabidhi Wilaya ya Bukombe.
Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga baada ya kuweka jiwe la Msingi kwenye ofisi za kata ya Busonzo.
Jiwe la Msingi

Viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wa Mwenge wakikagua Nyumba ya wahudumu wa afya Zilizopo kwenye kituo cha afya cha Uyovu.

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour ,akitoa ujumbe wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ambapo amesisitiza Watanzania Kujenga desturi ya kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kutumia ubunifu wa kubuni viwanda vidogo.
Baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa wamesimamishwa wakati kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru alipokuwa akitoa maelekezo.

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour ,akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Bara bara ya Uyovu Namonge yenye urefu wa Km,12.5 katika kijiji cha Bugege na Namonge ujenzi huo unatarajia kumalizika tarehe 15/9/2017.

Mbio za mwenge zikiendelea na kupita kwenye maeneo ya Wilaya ya Bukombe.

Kiongozi wa Mbio za mwenge akikagua mashine ya kukoboa mpunga pamoja na Mkurugenzi wa Kapalata Millers Investment .

Mkurugenzi wa Kapalata Millers Investment akielezea juu ya manufaa ambayo yameendelea kupatikana kutokana na uwepo wa mradi huo ambapo vijana 20 wameajiriwa kwenye kiwanda hicho wakiume wakiwa ni 10 na wakike 10,Kiongozi wa mbio za mwenge amepongeza uwekezaji wa namna hiyo na kwamba utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.


PICHA ZOTE NA JOEL MADUKA (MADUKA ONLINE)

No comments:

Post a Comment