Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi
katika wilaya ya Kondoa na Chemba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.James
Kiologwe na viongozi wa wilaya ya Chemba na Kondoa.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya za Kondoa na Chemba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
Wananchi waliofika katika uzinduzi wa hospitali tembezi.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Makatibu tawala wa mikoa yote
Tanzania bara kuratibu zoezi la Hospitali tembezi katika mikoa yao ili
kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kupata huduma ya kibingwa.
Jafo ametoa agizo hilo leo
alipokuwa akizindua huduma za hospitali tembezi kwa wilaya ya Chemba na
Kondoa zoezi ambalo limefanyikia mjini Kondoa.
Mpaka sasa zoezi hilo
limeshafanyika katika wilaya ya Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na sasa
linaendelea kwa wilaya za Chemba na Kondoa.
Akizindua huduma hiyo, Jafo
ameumwagia sifa uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kuratibu vyema zoezi
hilo ambapo zaidi ya wagonjwa 8,000 wamefanyiwa uchunguzi huku 500
wakifanyiwa upasuaji mdogo na mkubwa.
Amewataka wananchi wa wilaya hizo
kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa huku akiwataka
kupima tezi dume kwa kuwa umekuwa ugonjwa tishio kwa wanaume.
Ameeleza kuwa huduma hizo za kibingwa zinatolewa kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha wananchi wasio na uwezo kupata matibabu.
Jafo amewapongeza madaktari bingwa wa mkoa wa Dodoma kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewataka wengine waige mfano wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment