Saturday, August 12, 2017

DED MNASI: AKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI KATIKA HALMASHAURI YA ILEJE MKOANI SONGWE

Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Haji Mnasi akiwa anakagua mradi wa mfereji mkubwa wa umwagiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa wananchi wa Ileje akiwa Sambamba na viongozi na wananchi wakati wa ukaguzi.
Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akisikiliza maelezo ya mradi huo kutoka kwa wataalamu ambao pia ni wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Na fredy Mgunda, Ileje

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Leo amefanya ziara ya kushitukiza kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kutokana na ila ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015 kwenda 2020 chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM taifa.

Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ukaguzi  wa maendeleo ya ujenzi mfereji mkuu wa umwagiliaji wenye urefu wa km 6  wa sasenga maeneo ya kata ya mbebe lengo ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati na unawanugaisha wananchi wa vijiji vyote vya mradi.

"Mradi huu ni mkubwa sana naomba wananchi wautumie vizuri na kuutunza kwa kuwa unamanufaa ya muda mrefu kutokana na ujenzi wake kuwa mkubwa na wagharama kubwa na unaubora unaokidhi vigezo vyote kuwa mradi wa kutumu"alisema Mnasi

Mnasi aliwataka wananchi kuutunza na kuulinda mreji huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa katika ukanda huo wa halmashauri ya wilaya ya Ileje.

"Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje wametegemea Kilimo katika kuendesha maisha yao hivyo uwepo wa mradi huu utakuwa na tija ya kimaendeleo kwa wakulima na wafanyabiasha mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika halmashauri hii" alisema Mnasi

Aidha Mnasi aliwaomba wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe kuitumia vizuri fursa za uwepo wa mfereji mkubwa kwenye eneo hilo ambao unaweza kutumiwa kwa kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakuwa na tija kwa maendeleo yako.

"Wananchi wangu itumieni vizuri fulsa hii kuleta maendeleo katika halmashauri hii sihitaji kusikia malumbano yoyote juu ya matumizi ya mradi huu wa umwagiliaji ambao unatija sana kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla"alisema Mnasi

Mnasi alitoa onyo kwa wafugaji wenye mifugo yao husani ngombe ambao wamekuwaa wakizagaa katika eneo hilo ,alimwagiza mtendaji wa kata mwashitete kusimamia agizo hilo na kuongeza kinyume cha hapa mifugo hiyo itatozwa faini kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude aliwataka wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa serikali imefanya kazi kuwa kuwaletea maendeleo ya Kilimo kwa wakulima ili kupunguza idadi ya wananchi tegemezi.

"Unajua huu mfereji utaongeza ajira kutokana na Kilimo kinacholimwa katika wilaya hii hivyo ni lazima wananchi kuutunza na kuuthamini mradi huu" alisema mkude

Lakini mkude alimtaka Mkurugenzi na kamati zake kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu kwani serikali imetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kuinuka hapo mlipo kwenda hatua nyingine ya kimaendeleo.

"Mkurugenzi hakikisha kuwa huu mradi unasimamiwa vizuri na kuutunza ili uweze kudumu kwa muda mrefu kama lengo la serikali litimizwe kama ilivyopangwa"alisema mkude

Nao baadhi ya wananchi ambao niwakulima wameishukuru serikali kwa mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa Kilimo ndio maisha yao hivyo wanatarajia kunufaika na kukuza uchumi katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment