Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro amezindua mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia ‘GBV Prevention
Project’ unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice
of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za
kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu
Agosti 14,2017 katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga na
kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto wakiwemo
wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,maafisa watendaji wa
kata,maafisa tarafa,afisa maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii,afisa
utamaduni na dawati la jinsia na watoto.
Akizungumza wakati wa kuzindua mradio
huo,Matiro alilipongeza shirika hilo kwa kuelekeza nguvu zake katika
mapambano dhidhi ya ukatili wa kijinsia ambao unachangiwa kwa kiasi
kikubwa na jamii husika kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya
dola pale wahusika wanapobainika.
“Serikali inatambua kazi nzuri
zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali,ili mfanikiwe mnatakiwa
mshirikishe wadau kwenye maeneo husika,mmefanya jambo jema
kujitambulisha badala ya kuanza kutekeleza mradi kimya kimya kama baadhi
ya mashirika vile yamekuwa yakifanya hali inayowafanya washinde
kufanikiwa”,alieleza Matiro.
“Serikali ipo nanyi bega kwa bega,pale
mnapokwama tafadhali tupeni taarifa nasi tutawasaidia kadri
tutakavyoweza kwani lengo kuu ni kuwahudumia wananchi wetu ili kuzuia
vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa wanawake na watoto katika
jamii”,aliongeza Matiro.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo
kuyakumbusha mashirika na taasisi mbalimbali zinazotekeleza miradi
katika jamii kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la jadi
‘sungusungu’,viongozi wa kimila pamoja na watu mbalimbali wenye
ushawishi katika jamii husika.
Akitambulisha Mradi huo,Mkurugenzi wa
TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema mradi huo unaofadhiliwa na taasisi ya
kusaidia asasi zisizokuwa za kiserikali la The Foundation For Civil
Society unaolenga kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia
utatekelezwa katika kata tano katika wilaya ya Shinyanga ambazo ni
Usanda,Samuye,Nsalala,Tinde na Didia.
Ngangala alisema ili kutekeleza mradi
huo kikamilifu shirika hilo litashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo
viongozi serikali,dini,wananchi na wadau wengine.
“Matarajio yetu kupitia mradi huu ni
kwamba kufikia mwezi Januari mwaka 2018 kuwepo na mfumo mzuri wa kutoa
taarifa za ukatili wa kijinsia kutoka ngazi ya jamii hadi dawati la
jinsia kwa kushirikiana na maafisa utamaduni,maafisa watendaji,maafisa
maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii na mashirika mengine”,alieleza
Ngangala.
“TVMC ambayo walengwa wake wakuu ni
watoto na wanawake imekuwa ikishirikiana na serikali katika kutekeleza
majukumu yake ya kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na usalama ,elimu na
afya bora,msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto lakini pia matunzo
kwa watoto”,alieleza Ngangala.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi TVMC,Japhet Daud alisema kupitia mradi huo wataibua mijadala
kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia kupitia matamasha,michezo,ngoma
za asili,kutoa elimu na mbinu zingine kadha wa kadha. Katika hatua
nyingine Daud alisema ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni pamoja
na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoani Shinyanga ni vyema wadau wote
wakashiriki katika mapambano hayo badala ya kuiachia serikali pekee.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa
kijinsia unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice
of Marginalized Community (TVMC). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya
wakurugenzi TVMC,Japhet Daud,kushoto ni Afisa Mtendaji kata ya
Usanda,Emmanuel Maduhu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza ukumbini.
Wadau wa haki za watoto na wanawake wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la
kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas
Ngangala akitambulisha mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa
na shirika hilo.
wadau wakiandika dondoo muhimu.
Mkurugenzi wa TVMC ,Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi huo.
Wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa mradi huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi wa TVMC ,Mussa Jonas Ngangala akisisitiza jambo ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akielezea kuhusu mbinu mbalimbali watazozitumia katika kufanikisha mradi huo.
Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Kiongozi wa dawati la Jinsia na watoto
Shinyanga,Vivian Zabron akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa mradi wa
kuzuia ukatili wa kijinsia.
Wadau wakiwa ukumbini.
Afisa Utamaduni wilaya ya Shinyanga,Janeth Elias akichangia hoja ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment