Rais
Donald Trump wa Marekani amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani, John Kelly
kuwa mkuu wa utumishi wa Serikali baada ya kumwachisha kazi Reince
Priebus.
Priebus amefanya kazi kwenye Serikali hiyo kwa muda wa miezi sita tu.
Baada
ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatima ya Priebus, Trump ametangaza
uamuzi wake kwenye mtandao wa Twitter akiwasili mjini Washington.
Awali, Trump alitoa hotuba jijini New York ambayo aliitumia kummwagia sifa Kelly kwa kazi anayofanya katika wizara hiyo.
Amesema ,"Nina furaha kuwafahamisha nimemteua waziri John Kelly kuwa mkuu wa utumishi wa Serikali katika Ikulu."
No comments:
Post a Comment