Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaa Mhe Paul Makonda leo Julai 29, 2017 ameungana na wakazi wa jiji la Dar es salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers kwenye tamasha la wazi la KOMAA (maarufu Komaa Concert) linalo ratibiwa na kituo cha utangazaji cha EFM na Tv E
Katika salamu zake Mh Makonda amewasifu waandaaji wa tamasha hilo la aina yake lililofanyika mchana huu katika viwanja hivyo kwa ubunifu wa pekee.
Mh Makonda amewasihi waandaaji wengine kuiga mfano wa efm na Tv E wa kuandaa matamasha makubwa yanayogusa rika zote na kwa muda rafiki ambao hauleti kero kwa wakazi wa maeneo jirani tofauti na matamasha yaliyozoeleka yafanyikayo usiku ambayo ni kero kubwa kwa wakazi wanaozunguka kumbi na viwanja vinavyotumika mida hiyo ya usiku ambayo kwa kawaida ni mida ya mapumziko.
No comments:
Post a Comment