Saturday, July 1, 2017

NAIBU WAZIRI MPINA ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA NA KISHA AFANYA UKAGUZI KIWANDA CHA OK-PLASTIKI

Na: Hashim Jumbe


Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina, leo ameshiriki kwenye zoezi la usafi na Watumishi wa Manispaa ya Ilala ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya usafi wa mazingira iliyozinduliwa tarehe 9 Disemba, 2015 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Akiwa kwenye eneo la Mchikichini ambako kulifanyika zoezi la usafi asubuhi ya leo, Mhe. Luhaga Mpina alitoa maelekezo na maagizo mbalimbali kwa Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Mhe. Luhaga Mpina alianza kwa kutoa maelekezo kwa Viongozi wa Halmashauri kuwachukulia hatua Wananchi wote wasiojitokeza kushiriki usafi kwenye maeneo yao, kwani usafi ni lazima na siyo hiyari.

Aidha, Mhe. Mpina aliendelea kutoa maelekezo kwa Wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na Mfereji wa Mchikichini kutupa takataka katika maeneo waliyoelekezwa na Viongozi wao na siyo kwenye mfereji huo, huku akiwataka Wananchi hao kuacha mara moja kutiririsha maji taka kwenye mfereji huo na badala yake mfereji huo uendelee kufanyiwa usafi.

Katika maagizo aliyoyatoa Mhe. Mpina wakati akiongea na Wananchi wa Kata ya Mchikichini na maeneo ya jirani, Naibu Waziri huyo aliagiza yafuatayo;

Mosi, kuanzia sasa orodha ya Watu wote waliounganisha mifumo yao ya utiririshaji wa maji taka na Mfereji wa Mchikichiki, Halmashauri iwachukuliwe hatua mara moja, na wale mtakaowashindwa ndiyo mtuletee

Pili, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala nakuagiza kutenga eneo la kuhifadhia taka kama vile matairi, mzihifadhi kwa muda wakati Serikali tunatafuta suluhu ya kudumu.

Tatu, tunapozalisha taka tujue ni mali, na wale wote wanaobadilisha taka kuwa mali wajitangaze ili Wananchi wajue wapi watazileta taka hizo.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mpina alipata nafasi yakutembelea kiwanda kinacholalamikiwa na Wananchi wa Vingunguti kwa uchafuzi wa mazingira, kiwanda cha cha OK-Plastiki na baada ya kufanya ukaguzi kwenye kiwanda hicho, Mhe. Mpina alitoa maelekzo, maagizo na ushauri.

Upande wa maelekezo, Mhe. Mpina aliielekeza Mamlaka inayosimamia mazingira 'NEMC' kuhakikisha kila baada ya miezi mitatu inafanya ukaguzi na kuangalia kiwango cha moshi unaotolewa kwenye kiwanda hicho.

Maagizo yaliyotolewa na Mhe. Mpina ni kama yafuatayo;

Mosi, Kiwanda cha OK-Plastiki na NEMC wahakikishe wanapata kiwango cha moshi unaotelewa kwenye kiwanda hicho na matokeo niyapate tarehe 15 Julai,2017

Pili, kabla ya hiyo tarehe 15 Julai, NEMC lazima wajue kiwanda kinazalisha bidhaa waliyoomba kuzalisha? na kama kuna bidhaa wameiongeza, je walifuata taratibu?

Tatu, ndani ya siku hizo 15 kiwanda kama mnaweza kupunguza dosari zilizopo kwa kuboersha miundombinu yenu ya kiuzalishaji fanyeni hivyo, maana nikija hiyo tarehe 15 Julai kukiwa na kasoro nitakifunga kiwanda.

Mwisho, Mhe. Mpina alitoa ushauri kwa kiwanda hicho kuangalia namna ya kuwafidia Wananchi waliokaribu na maeneo ya kiwanda na Serikali kusimamia zoezi la uthamini naulipaji fidia












Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Ndugu Edward Mpogolo kushoto akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina














No comments:

Post a Comment