Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Elisha Mghwira Julai 12, 2017 amezindua Baraza la uwezeshaji Wanawake kiuchumi lililofanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Mhe Mghwira amezindua Baraza hilo ambapo kabla alianza Kwa kutembelea maonyesho ya shughuli zinazofanywa na Wanawake na Taasisi zinazowezesha Wanawake.
Akizungumza mara baada ya kutembelea shughuli hizo alisema kuwa amefurahishwa na hatua kubwa iliyofikiwa na wanawake Kwa ubora wa bidhaa wanazozalisha.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Aliagiza kuwa kufikia mwaka 2018 Mkoa wa Kilimanjaro unatakiwa uwe na banda la Maonyesho katika maonyesho ya Saba Saba na Wanawake wawezeshwe ili wahudhurie maonyesho hayo na kutangaza biashara na bidhaa zao.
Pia Alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kuongeza juhudi katika kukusanya mapato ili waongeze kiasi wanachowakopesha Wanawake hao toka kwenye mapato ya ndani.
"Ikiwezekana Kikundi chenye watu watano kipewe Milioni kumi ili kila mwanakikundi apate walau shilingi milioni mbili, badala ya Shilingi Milinoni mbili na laki tano wanazopata Sasa Kwa Kikundi kizima" Alisema Mhe Mghwira
Sambamba na hayo pia Alipongeza Halmashauri ya Wilaya na hasa idara ya maendeleo ya Jamii Kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Mhe Mghwira Amewasihi Wanawake kuendelea kukuza biashara zao ili kuachana na utegemezi ambapo pia inapelekea kupunguza unyanyasaji katika familia.
Kwa upande wa wanaume Aliwaasa kuwa karibu na wake zao na kuwapa moyo ili kujenga familia Imara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule akitoa ufafanuzi wa uzinduzi huo, alieleza jinsi Wilaya hiyo inavyoshirikiana kwa karibu na wanawake hao wakati wote Pamoja na mipango iliyopo kwa ajili ya kuwajengea uwezo zaidi wanawake hao.
Katika uzinduzi huo Taasisi za uwekezaji zilizohudhuria ni pamoja na TRA, NMB benki, PPF, Same SACCOS, Same Councelling, Roman Catholic idara ya wanawake nk.
Nao baadhi ya Wanawake kwa niaba ya wengine walimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa na kumuahidi kumpa ushirikiano na kumtakia utekelezaji mwema katika majukumu yake.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA SAMEMkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Elisha Mghwira akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la uwezeshaji Wanawake kiuchumi lililofanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Elisha Mghwira akisalimiana na viongozi mbalimbali Mara baada ya kuzuru kuzindua Baraza la uwezeshaji Wanawake kiuchumi lililofanyika Wilayani Same.Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule akitoa ufafanuzi wa uzinduzi wa Baraza la wanawake Wilayani humo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira
No comments:
Post a Comment