Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amehudhuria mashindano ya kumsaka mlimbwende wa Jimbo la Ilemela kwa mwaka wa 2017 yaliyofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza
Akizungumza katika mashindano hayo Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa ataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuibua vipaji vipya vya vijana wa Jimbo la Ilemela sambamba na kuviendeleza vile vya zamani walivyonavyo vijana hao lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kila mmoja ananufaika na kipaji alichonacho sambamba na kujikwamua kiuchumi kupitia kipaji alichonacho
‘… Niwaombe tuzidi kushirikiana kuhakikisha tunaibua vipaji vipya walivyonavyo vijana wetu sambamba na kuendeleza vila vya awali, Tukifanya hivi tutakuwa tumeanzisha namna mpya ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kama ninavyosema mara zote michezo ni afya lakini michezo ni ajira …’
Wakati huo huo Mbunge huyo pia ameshiriki mahafali ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kupitia Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu kwa Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika ukumbi huo huo wa Rock City Mall huku Mgeni Rasmi akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara Comred Rodrick Mpogolo akiambatana na Viongozi wengine akiwemo M/kiti wa CCM Mwanza Comred Antony Dialo, Katibu wa CCM Mkoa Mwanza Comred Raymond Mwalimu, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula na wengineo
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.07.2017
No comments:
Post a Comment