Na; Abdul O. Nondo
Habari watanzania kabla ya yote tuanze angalia nini maana ya mswada na mswada wa Dharura (bill under certificate of urgency)
Mswada ni mapendekezo ya sheria yaliyo katika mchakato wa kuwa sheria, (draft of proposed act).kuna aina mbili ya miswada
1.mswada binafsi (private bill) unaowasilishwa mara nyingi na wabunge, huu hauwekwi katika gazeti la serikali.
2.mswada wa serikali(government bill).unaoandaliwa na serikali eidha kupitia waziri au mwanasheria mkuu huu wekwa katika gazeti la serikali baada ya kutoka hatua yake ya green paper na light paper ambazo hatua
hizi huwa huwa zipo ktk ministerial level, permanent secretariate na baraza la mawaziri.
Huwekwa katika gazeti la serikali siku 21 kabla ya kupelekwa bungeni kwa hatua kadhaa kadhaa hii huwapa wabunge muda wa kujiandaa na kusoma mswaada vizuri zaidi ila Kama ni mswada wa hati ya Dharura (the bill under certificate of urgency BCU)hauwekwi katika gazeti hupelekwa moja kwa moja bungeni kwa majadiliano zaidi na huwa haitoi muda zaidi kwa maadalizi mswada huu ndio huitwa *maswada wa hati ya dharura /bill under certificate of urgency*
*JE WANAOPINGA MSWADA WA RASILIMALI ULIOPELEKWA BUNGENI WANA HAKI YA KUPINGA SABABU YA MUDA*
kuna sababu mbili tuu ambazo hufanya serikali kupeleka miswada kwa hati ya dharura, *Time related reason*(sababu ya mahusiano ya muda ) and *content related reason*(sababu ya maudhui)
Time related reason ni pale serikali inapeleka haraka haraka, ili bunge lihairishwe sababu ya tukio linalokuja (upcoming events) labda uchaguzi, sikukuu, kuwahi mwaka wa fedha (fiscal date). Lakini sababu hii haingii kwa kuletwa mswada wa hati ya dharura, sababu hakuna tukio, wala muda tunaokimbizana nao.
2 *content related reason* hii ni kuhusu maudhui ya mswada wenyewe, maudhui yanaweza kuwa ni yanayopigiwa kelele kila siku na watu, raia, taasisi, viongozi, wanataka yabadilishwe, hii hufanya serikali kusikia sauti hizi nakuamua kupeleka haraka kwa hati ya dharura,hii ndio ilivyotokea kwa miswada hii ya rasilimali ndio maana imepelekwa kwa hati ya dharura.
Je, hii miswada inahitaji muda tena?, kwa mambo ambayo nyie wabunge, taasisi, jamii mlikuwa mnapigia kelele, inahitaji muda, muda wa nini?
Kwa mbunge makini hawezi dai muda zaidi, sababu ni mambo ambayo yapo wazi, na tayar watu wanamapendekezo yake muda mrefu, mfano.2012 kafulila, machali, mbowe ,mbatia walikuwa wakipiga kelele juu ya umiliki wa rasilimali, tundu lisu amekuwa akipiga kelele juu ya mikataba mibovu na usiri, na Ukisoma kitabu cha *ASEMAVYO ZITTO* kuanzia ukurasa wa 172.imeelezea kila kitu *Tanzania bila laana ya rasilimali*, *utajiri wa nchi ni mali ya nani*, hii ina maana matatizo yanajulikana na kwa sababu mmekuwa mkilaumu basi natumai mapendekezo lazima muwe nayo Hakuna haja ya muda zaidi wa nini??
Hivi mswada, unaotaka rasilimali kuwa mali ya wananchi kupitia serikali 1. *natural wealth and resources(permanent sovereignty)act 2017* hivi mswada huu unahitaji muda zaidi?
2.hivi mswada unaohitaji mikataba yote kuhidhinishwa na bunge, *natural weath and resources contracts act 2017* hivi na mswada huu unahitaji muda kweli?
3.mswada unaotaka chombo cha usimamizi rasilimali *written laws( miscellaneous amendment act 2017*)
Maana ya kupewa muda wa kutosha ni kupata wasaa kujadili, kuandaa mapendekezo, swali unataka kujiandaa nini ikiwa siku zote umekuwa bungeni ukiishauri serikali, na ukitoa mapendekezo yako juu ya mambo haya leo yanaletwa unataka muda wa nini ?
Au labda ulikuwa unakosoa na kushauri usichokijua?
Miswada ya inayotakiwa pingwa under certificate of urgency ni ule wa vyombo vya habari *media service bill*,sababu ulihitaji consultations kubwa na stakeholders, pia uelewa kwa wabunge lakini sio huu wa rasilimali.
1989,New Zealand,katika bunge lake la 49,walipitisha miswada 23 under certificate of urgency (hati ya dharura), wabunge walipinga kwa kusema kuna miswada haihitaji haraka wakaitoa ilikuwa *environment canter bury act*, *Employment relation(film production work) amendment act* wakidai inahitaji ufaham na majadiliano ya kina, miswada iliyobaki walipitisha kwa hati ya dharura sababu ilikuwa inaeleweka.
Je, miswada hii ya rasilimali kwa hati ya dharura haieleweki kwa wanaopinga?
Jibu baki Nalo.
Abdul .O. Nondo.
0659366125/0762082783.
No comments:
Post a Comment