Sunday, July 16, 2017

KAIMU NAIBU UVCCM ZANZIBAR AKUTANA NA WALIOJAZA FOMU NGAZI YA TAIFA

Na mwandishi wetu Zanzibar.

Kaimu naibu katibu mkuu UVCCM ZNZ amekutana na waliojaza fomu wote kuomba ridhaa ya kuwa wagombea kwa nafasi mbali mbali za UVCCM ngazi ya taifa.

Tumewaiteni hapa kwa lengo la kukumbushana machache ambao hamruhusiwi kufanya Mara baada ya kujaza na kurejesha fomu kwa muda huu kazi yenu imeeisha hamruhusiwi kupita pita kwa nia au zamira ya kufanya kampeni.

Mnatakiwa mtulie msubiri vikao vya mapendekezo na vya maamuzi juu yenu majina yatakapo rudi nyote mtapewa barua za uteuzi na hapo mtaruhusiwa kufanya kampeni alisema Abdullgjafar.

Kaimu naibu Zanzibar pia aliwakumbusha swala zima la kujiandaa na vikao ambavyo watalazimika kuwepo wao kama wagombea na vikao hivyo hadi sasa havijajulikana vitafanyika wapi ila jambo la msingi kwao waaze kuchanga nauli maana hawatapewa nauli ya kwenda wala kurudi watakapo itwa na itakuwa aibu kwa mgombea kukosa kwenda kwenye vikao vya kujadiliwa kisa hana nauli au ameambiwa hafla.

Jumla ya wanachama wa umoja wa vijana wa CCM 83 kwa upande wa Zanzibar wamejitokeza kujaza fomu na waliorejesha ni 62 na mbili kwa nafasi mbali mbali hilo ni ongezeko kubwa sana ukilinganisha na miaka 5 iliyopita kwa mwaka huu vijana wamehamasika sana kwa ngazi zote kuazia shina tawi wadi jimbo wilaya na Mkoa.

Kaimu Abdullghafar mwisho aliwaagiza makatibu wa wilaya na Mkoa nao kufikisha maagizo hayo kwa waliojaza fomu kwa ngazi zao husika.

No comments:

Post a Comment