Na Mathias Canal, Mwanza
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka amefanya mahojiano na Lake Fm Radio ya Jijini Mwanza akielezea mambo Mbalimbali yahusuyo Ziara yake katika Mkoa wa Mwanza na umuhimu wa kukutana na wanachama wa CCM kwenye mikutano ya ndani.
"Chama Cha Mapinduzi Kina wajibu Mkubwa wa kuwapika Vijana kifikra, Kimwili na kiakili" Shaka
"Kila jambo Lina Wakati wake yawezekana tumetofautiana namna ya kiutendaji lakini maswala ya ubadhilifu na uhujumu uchumi hayakuanza kuchukuliwa Hatua Jana wala leo Bali kwa sasa tumetilia mkazo zaidi" Shaka
"UVCCM katika miaka ya hivi karibuni imeongoza majukumu yake ya kimsingi kuwasemea watanzania na kuikosoa Serikali pale inapokosea" Shaka
"Tumeendelea kuisimamia Serikali kwa weledi chini ya Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt John Pombe Magufuli hivyo Leo tumetangaza vita dhidi ya Halmashauri zote nchini zisizotoa asilimia 5 za mikopo kwa Vijana ilihali imeainishwa kwenye Ilani ya ushindi ya Mwaka 2015-2020" Shaka
"Katika Halmashauri zote ambazo tumetembelea tumejionea malalamiko ya Vijana kwa kutopatikana asilimia 5 kwa ajili ya Vijana na hata hela ambayo inatoka sio ile ambayo imeainishwa na Serikali" Shaka
"Zaidi ya milioni 395 ambazo zimetengwa kwa ajili ya makundi ya Vijana na Wanawake katika Wilaya ya Ilemela zaidi ya Milioni 90 zimeshatolewa na nimejionea mwenyewe Wakati wa Ziara yangu, Hivyo Halmashauri hii inapaswa kupongezwa na Halmashauri zingine kuiga jambo hilo" Shaka
"Katika uchaguzi Mkuu unaotaraji kufanyika Mwishoni mwa mwaka huu UVCCM tutaendelea kuwa imara zaidi kwa kupata viongozi bora na Mwenye weledi Mkubwa" Shaka
"Sisi Chama Cha Mapinduzi tunaheshimu sheria na taratibu za nchi ndio maana tunafanya mikutano ya ndani kama maelekezo ya Serikali yalivyosema kutofanya mikutano ya nje" Shaka
"Wenzetu hawana mitaji ya Sera na ilani badala yake wamekuwa watu wakupindisha maana tu kwa wananchi, Tofauti yetu na vyama vingine sisi ni chama cha siasa na wenzetu hatujui kama ni SACCOS ama vijiwe vya siasa" Shaka
"Hatutamvumilia mtu anayepanga safu katika uchaguzi wa ndani wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi" Shaka
"Umoja wa Vijana ndio taasisi ambayo imetoa Vijana wenye weledi mkubwa na wameweza kushika nyadhifa Mbalimbali za Uongozi katika chama na serikali na wameleta heshima kubwa ndani ya UVCCM" Shaka
"Tusipoteze kauli njema ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ya kutaka Chipukizi iboreshwe kwa ajili ya maandalizi mazuri ya Kujiunga na UVCCM muda utakapowadia" Shaka
"Kazi ya kuandaa Vijana kuwa viongozi mahiri inaendelea ndani ya UVCCM na hivi karibuni Vijana wataanza kupata mafunzo katika chuo chetu cha Ihemi Mkoani Iringa" Shaka
"Vijana wengi waliopewa dhamana ya kuwa wabunge na wapo Bungeni Mjini Dodoma kutimiza wajibu wao waachwe wawajibike vyema maana pale ni mahala pa ulingo wa Demokrasia" Shaka
"Sasa hivi Demokrasia imeimarika kwa kiasi kikubwa kwa kuheshimu sheria na taratibu za nchi, Ukikosoa katika misingi ya utaratibu hakuna mtu atakubuguzi" Shaka
"Baada ya kuasisiwa Taifa hili Lina Tunu zake kubwa na muhimu ikiwemo Amani, Upendo na Mshikamano" Shaka
"Tukosoe na kutoa ushauri dhidi ya nchi yetu katika kujenga chi na sio kukosoa kwa kuichafua Serikali kwa kutumia kejeli" Shaka
No comments:
Post a Comment