Wednesday, July 19, 2017

DC HOMERA AKAMATA MALORI MAWILI YA DANGOTE YAKIWA YANAINGIZA NGOMBE ZAIDI YA 75 WILAYANI TUNDURU KINYUME CHA SHERIA

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera amefanikiwa kukamata malori mawili ya kampuni ya Dangote yenye namba za usajili T 159 DKA na tela T 833 DKA ikiendeshwa na dereva Hamisi Hemedi ambaye alisimamishwa na kukadi kusimama katika geti la sauti moja na kwenda kushusha ngombe 40 eneo la mkowela.

Na gari la pili yenye usajili wa namba T 217 DKA na tela namba T 976 DKA chini ya dereva Emmanuel Musa Rajabu ambalo lilikutwa na zaidi ya ngombe 35 hivyo jumla ya ngombe zilizo bebwa na malori mawili ni zaidi ya 75 ambao waliletwa Tunduru kwa kigezo cha kuja kuchinjwa.

Akizungumza katika eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Tunduru alisema, anatoa rai kwa wafugaji wote walioko wilayani kibiti mkoa wa pwani na sehemu zingine wasiendele kuleta ngombe wilayani tunduru kwa kuwa tunduru haipokei mifugo, watakao leta watafikishwa mahakamani kama hawa watakavyofikishwa kesho(Leo).

Madereva wote wawili walikamatwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi Tunduru, dereva Hamisi Hemedi na Emmanuel Mussa Rajab pamoja na mmiliki wa ngombe hizo bw. Thobias John.

Aidha Dc Homera alimkamata wakala wa kuingiza mifugo wilayani tunduru kwa kutumia vibali feki bw. Daudi Athumani, huwa anadanganya anawaleta kwa ajili ya kuchinja ila huwa anawashusha njiani na kuwaingiza porini.

Nae msaidizi wa afisa mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru ndg. Fred mushi,  Dc Homera aliagiza akamatwe kwa kosa la kumdanganya na kushinikiza walio kamatwa waachiwe kwa kuwa ngombe hao wanavibali na Dc Homera alipomuhoji kwa kina alionekana hajui hata ngombe hao walipotoka na wanapo kwenda.

No comments:

Post a Comment