Wednesday, June 28, 2017

WATAALAMU WA KILIMO KUTOKA MANISPAA YA UBUNGO WAENDELEA KUPATA MAFUNZO NCHINI KOREA KUSINI

Gyeongsangnam, Korea Kusini

Wataalamu wawili wa masuala ya kilimo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo leo wameendelea kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa nchini Korea Kusini.

Wataalamu hao ambao ni Afisa Kilimo wa Manispaa hiyo Ndg. Salim Msuya na Bi. Stella Nzelu wanaendelea kupata mafunzo hayo katika jimbo la Gyeongsangnam lililopo Korea Kusini.

Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa kwa pamoja kati ya KOICA na jimbo la Gyeongsangnam  yanaingia siku ya tatu leo ambapo mafunzo  ya kitalu nyumba (green house production), kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, udhibiti wa magonjwa na wadudu wa mimea, kilimo mjini na uzalishaji wa zao la mpunga yanaendelea kutolewa.

Katika mafunzo hayo wataalamu hao kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo  wameandamana na maafisa kilimo wengine kutoka Manispaa za Ilala,  Temeke, Kigamboni, Kinondoni na Ofisi ya RAS.

IMETOLEWA NA;

KUTENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

No comments:

Post a Comment