Wednesday, June 28, 2017

WANANCHI WAMPIGIA MAGOTI MHE RITHA KABATI WA CCM WAMUOMBA MAJI

Na; Ramadhani Shabani

Ndugu Mtanzania Ni Tumaini Langu Wewe Ni Buheri Wa Afya Na Unaendelea Vyema Na Utekelezaji Mwema Wa Majukumu Yako Ktk Kulitumikia Taifa Letu Kwa Utekelezaji Wa Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi Tu!

Ndugu Mtanzania Kama Ilivyo Hada Yetu Ya Kukuletea Taarifa Za Mambo Mbalimbali Yanayojili Ktk Jamii Yetu,Sasa Na Leo Nimekuletea Hii Kutoka Wilayani Iringa Mjini Mkoani Iringa.

Wakazi Wa Mji Wa Tangamenda Wilayani Iringa Mjini Wameamuwa Kuandamana Kwa Kitendo Cha Makazi Yao Hayo Kukosa Maji Na Umeme Kwa Zaidi Ya Miaka Mitatu Sasa Huku Wakidai Kubaguliwa Na Serikali Ya Halmashauri Iliyopo Madarakani Sasa Inayoendeshwa Na Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA).

Wakizungumza Na Waandishi Wa Habari Waliokuwa Wameongozana Na Mhe Mbunge Wa Viti Maalum CCM Mkoa Wa Iringa Ritha Kabati Wananchi Hao Walisema Kwamba Wameamuwa Kuandamana Kupaza Sauti Yao Na Kusema Kinachowakuta Huku Kwao Ktk Kata Ya Ipogolo Ambayo Pia Inashikiliwa Na CHADEMA Huku Wakisema Endapo Halmashauri Itashindwa Kuwaletea Maji Safari Hii Basi Hawapo Tayari Kupiga Kura Ktk Uchaguzi Ujao Wa Mwaka 2020 Kutokana Na Kudai Halmashauri Hiyo Inayoongozwa Na CHADEMA Imewasahahi Kabisa Ktk Kuwaletea Huduma Muhimu Karibu Lakini Kwenye Ukusanyaji Wa Kodi Za Majengo Wamekuwa Wepesi Mno Kuja Kuchukua.

Wakizungumza Na Waandishi Wa Habari Mbele Ya Mbunge Wa Viti Maalum CCM Mkoa Wa Iringa Mhe Ritha Kabati Wananchi Hao Wanaume Kwa Wanawake Walisema Kwamba Wamechoshwa Na Kunywa Maji Pamoja Na Ngombe,Wamechoshwa Kunywa Maji Ambayo Wamekuwa Wakikuta Mizoga Na Maiti Muda Mwingine Lakini Zaidi Wamesema Wamechoshwa Na Kitendo Cha Kubakwa Kwa Watoto Pamoja Na Wanawake Wanapokuwa Wanaenda Kufata Maji Mtoni Ruaha.

Wakizungumza Kwa Jazba Wananchi Hawa Walisema Kwamba Walijazibika Mno Pale Walipo Msikia Mbunge Wao Mchungaji Msigwa Bungeni Akisema Kwamba Eti Wananchi Wa Iringa Hatuna Shida Ya Maji Wala Umeme Wakati Wakati Wao Wanateseka Kwa Ukosefu Wa Maji Na Umeme Na Mbaya Zaidi Wanasema Aliishawahi Kuwatembelea Na Kujionea Shida Ya Maji Waliyonayo Sasa Leo Wameshangazwa Na Yeye Aliposimama Bungeni Na Kusema Kwamba Iringa Mjini Wananchi Wake Hatuna Shida Ya Maji Wala Umeme.

Wananchi Hao Wakizungumza Kwa Uchungu Na Udhuni Kubwa Waliamuwa Kumpigia Magoti Mbunge Wa Viti Maalum CCM Mkoa Wa Iringa Mhe Ritha Kabati Huku Wakimwambia Na Yeye Akishindwa Kuwasikiliza Na Kuwasaidia Kutatua Hiyo Kero Basi Hawatakuwa Na Sehemu Ya Kimbilio Tena,Na Hivyo Kumpigia Magoti Mhe Ritha Kabati Awasaidie.

Akizungumza Mhe Ritha Kabati Baada Ya Kuwasikiliza Wananchi Hao Alisema Binafsi Niwape Pole Sana Kwa Usumbufu Mkubwa Ambao Mmekuwa Mkiupata Kutokana Na Kero Hii Ya Maji Na Umeme Kwani Ni Wanawake Wenzangu Ndio Mmekuwa Mkipata Hii Hadha,Lakini Pia Kutokana Na Hali Nazidi Kujiuliza Na Kushangazwa Sambamba Na Kutiwa Udhuni Kwani Mbunge Mwenzangu Wa Jimbo Hili Mchungaji Msigwa CHADEMA Aliposimama Juzi Mbungeni Alisema Kwamba Jimboni Kwake Hapa Wananchi Wa Iringa Mjini Hamna Shida Ya Maji Wala Umeme Wakati Kumbe Kuna Wananchi Tena Ambao Anafahamu Shida Yao Wanapata Tabu Kwa Kukosa Maji Safi.

Baada Ya Kuzungumza Hayo Yote Mhe Ritha Kabati Aliwaahidi Wananchi Hao Kulifanyia Kazi Hilo Tatizo Lao Na Hivyo Baada Ya Kutoka Hapo Mhe Mbunge Huyo Alielekea Moja Kwa Moja Mbaka Ofisini Kwa Mkurugenzi Wa Halmashauri Hiyo Ambapo Kwa Bahati Nzuri Licha Ya Jana Kutokuwa Siku Ya Kazi Kutokana Na Mwendelezo Wa Sikukuu Ya Eid Pili Lakini Mkurugenzi Huyo Alikuwepo Karibu Na Maeneo Ya Ofisi Yake Ndipo Mhe Ritha Kabati Akachukua Fursa Hiyo Kumuomba Awasaidie Wananchi Wale Na Awapelekee Maji Na Mkurugenzi Yule Alimwambia Wapo Kwenye Huo Mpango Mkakati Wakuwapelekea Maji Safi Na Salama Wananchi Wale Huku Akimuomba Mhe Ritha Kabati Kuandika Barua Ambayo Itakayosukuma Zaidi Kasi Ya Kupeleka Maji Na Umeme Ktk Eneo Lile La Mtaa Wa Tagamenda Ktk Kata Ya Ipogolo.

Ndugu Mtanzania Kiongozi Bora Ni Yule Anayefanya Kazi Ile Anayoagizwa Na Wananchi Wake Akaifanye,Lakini Pia Kiongozi Bora Ni Yule Anayeona Wananchi Wake Wakiumizwa Na Kuamuwa Kuwasikiliza Na Kutafuta Suluhu Ya Kukomesha Tatizo Hilo Kwa Wananchi Wake Sambamba Na Hili Kiongozi Makini Ni Yule Ambaye Ni Mnyenyekevu Na Msikivu Kwa Wananchi Wake *Mhe Ritha Kabati* Hata Mimi Niliyeogozana Nawe Mkoani Iringa Kwenye Ziara Yako Nimejionea Namna Ambavyo Unaguswa Moja Kwa Moja Na Shida Sambamba Na Matatizo Ya Wananchi Wa Iringa.

No comments:

Post a Comment