Serikali
imetoa siku saba kwa ajili ya halmashauri zote kuhakikisha walimu wa
hesabu, sayansi na wataalamu wa maabara waliopangwa hivi karibuni
wanapewa posho za kujikimu.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki
alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema).
Mkundi
alitaka kujua ni lini serikali itawalipa stahiki zao walimu wa Hesabu,
Sayansi na watalaamu wa maabara waliopangiwa vituo hivi karibuni.
Alisema halmashauri zote zilizopokea walimu hao zinapaswa kuwapa posho za kujikimu ndani ya siku saba.
Akijibu
swali la msingi la Mkundi aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa
kutoa posho za mazingira magumu kwa watumishi wa maeneo ya pembezoni,
alisema, “Katika kutekeleza Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha
iliyopitishwa mwaka 2010, mwaka 2012/13 halmashauri 33 za wilaya ikiwemo
halmashauri ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo ya kutoa motosha
kwa watumishi.”
Alisema
kutokana na mpango huo, halmashauri 29 ziliandaa na kuwasilisha katika
ofisi ya wizara hiyo miongozo iliyobainisha aina ya motisha
inayohitajika.
“Utekelezaji
wa miongozo hiyo kwa halmashauri zote 29 ulikadiriwa kugharimu Sh
bilioni 331.087 kwa mwaka na utekelezaji wa miongozo hiyo, ulitarajiwa
kuanza katika mwaka wa fedha wa 2013/14 na haukuanza kutokana na ufinyu
wa bajeti."
No comments:
Post a Comment