Saturday, June 24, 2017

NSSF YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 1.5 UPANUZI WA KIWANDA CHA CHAKI SIMIYU

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu,  fedha ambazo ni  mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Chaki Wilayani humo na kuongeza uzalishaji.
Hundi hiyo imekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa vitendo  na kuwataka viongozi wa mkoa huo kutokatishwa tamaa.
Amesema NSSF kama Shirika la Umma linatekeleza sera na maelekezo ya Serikali na wametoa mkopo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ili wafanye upanuzi wa kiwanda cha chaki na kuongeza uzalshaji kwa kuwa suala la Viwanda ni la kipaumbele.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na  watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema kiwanda cha Chaki Maswa kimebeba ujumbe na dhana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kushikamanisha Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya watu kwa sababu kinatumia malighafi ya hapa nchini.
Aidha, amesema kiwanda hiki kitawanufaisha Watanzania hususani vijana wa Mkoa wa Simiyu ambao watafanya kazi moja moja katika kiwanda na wale wataohusika katika uchimbaji wa malighafi ambayo inapatikana maeneo mengine  hapa nchini.
Asilimia 56 ya nguvukazi hapa Tanzania ni vijana na vijana wengi bado hawana ajira lakini kiwanda hiki kitasaidia, kwa kuwa sehemu ya hiyo asilimia 56 wataajiriwa katika kiwanda na wengine watapata ajira huko mkoani Singida ambako malighafi ya kutengenezea chaki inapatikana” amesema.
Mhe.Mhagama ameongeza kuwa kiwanda kitatatua tatizo la upatikanaji wa chaki hapa nchini,kitaokoa fedha kwa kuwa chaki zitauzwa kwa bei nafuu na kitaongeza mapato ya fedha za kigeni kwa kuwa chaki zitakazozalishwa zitauzwa katika soko la nje ya nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeonesha mfano katika kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli la kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa kujenga kiwanda hicho kikubwa, ambapo amesema kufikia mwaka 2020 Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitakuwa mfano kwa kuwa na miradi yake zenyewe .
     “Kama Halmashauri zinakopa mabilioni kujenga stendi, masoko kwa nini zisikope kujenga viwanda, zikatumia malighafi ya hapa nchini  zikaajiri Watanzania wakapata kipato na nchi yetu ikanufaika; Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitaajiri na kwenye miaka mitano ya Mhe.Rais tutatoa mfano wa kuwa Halmashauri zenye miradi yake” amesema.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mhe.Riziki Pembe Juma amesema Zanzibar ni wadau wakubwa wa Chaki zinazotengenezwa Maswa(Maswa Chalks), hivyo ameomba ushirikiano ulioanzishwa kati ya Zanzibar na Simiyu udumu ili kufikia malengo katika kukuza kiwango cha elimu na utekelezaji wa Sera ya Viwanda.

Kiwanda cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa kwa sasa kinazalisha katoni zaidi ya 180 kwa siku na chaki hizo zinatumika katika shule zilizopo katika maeneo tofauti hapa nchini,  ikiwa ni pamoja na mikoa yote za Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ikiwemo Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita na Tabora.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama(kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kushoto), viongozi wa Wilaya ya Maswa wakimkabidhi Meneja wa Benki ya Azania( wa pili kulia) Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki wilayani humo ili aendelee na taratibu za kibenki.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara(kulia)  wakiteta jambo wakati wa hafya ya makabidhiano ya hundi  ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Wilayani Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama(wa tatu kulia), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi (wa pili kulia)katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa, wilaya ya Maswa na Vijana wa Maswa Family wanaofanya kazi katika kiwanda cha chaki.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa ya Upembuzi yakinifu wa panuzi wa kiwanda cha chaki cha Maswa kutoka kwa mtalaam wa Taasisi ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Deodatus Sagamiko.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mhe.Riziki Pembe Juma akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama( wa pili kushoto) akiangalia kikundi cha ngoma mara mara baada ya kuwasilisi wilayani Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya Hundi yashilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Msanii Elizabeth Maliganya (kulia) na baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi (wenye sare za vitenge) wakicheza na viongozi mbalimbali mara baada ya makabidhiano ya hundi  ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama(wa tano kulia), Waziri wa Elimu Zanzibar (mwenye ushungi mwekundu), mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa sita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Maswa na wadau wengine wa maendeleo baada ya makabidhiaono ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na viongoziwa mkoa na wakuu wa idara wa Halmasahuri ya Wilaya ya Maswa baada ya makabidhiaono ya Hundi yashilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Maswa Mashariki, mhe.Stanslaus Nyongo mara baada ya kuwasili wilayani Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamau za mkoa wakati wa hafla ya makabidhiano yaHundi ya shilingi bilioni 1.5 iliyotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Baadhi ya viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.

Baadhi ya viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara(mara baada ya kuwasili wilayani Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.

No comments:

Post a Comment