Sunday, June 25, 2017

MWENYEKITI WA PONDEZA FOUNDTION APANIA KUINYANYUWA TAASISI HIYO

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mwenyekiti wa taasisi ya PONDEZA FOUNDTION inayo jishuhulisha na malezi ya watoto yatima kukuza elimu kusaidia watoto wenye mazingira magumu na kuwasaidia kujikomboa kiuchumi elimu na ujasiriamali.

Tunalea watoto yatima chini ya miaka 18 na wakifika umri huo majukumu tunayaelekeza kwa wazazi wao hadi Sasa tunao watoto 360 tunalea.

Mimi kama Mwenyekiti nimekusadia kwa dhati kuwakomba vijana kupitia taasisi yetu nina marafiki wengi ambao wapo tayari kuisaidia taasisi baada ya kuitambulisha kwao na kuona kazi za taasisi kuwa zinaeleweka na zinasaidia jamii alisema Mh Pondeza.

Katika marafiki walio tayari kuisaidia taasisi ipige hatuwa ni rafiki yangu Moyor wa Jiji la Washington Marekani nimepata mualiko nitakuwa USA 9/07/2017 nitakuwa na mazunguzo na Moyor wa jiji la Washington na 10/07/2017 tutakuwa na mazungumzo na watazania wanaoishi Marekani lengo la maongezi hayo ni kuwa tayari kuisaidia taasisi yetu ili iwakombowe vijana.

Mh Pondeza amesema Zanzibar inaweza kuachana na kuagiza bidhaa nyingi za kilimo hasa cha mboga mboga na matunda alisema program nyingi za kilimo zipo tena cha kisasa wataalum wapo wakigeni na wazawa ila changamoto kubwa ni ardhi nina miaka miwili tangu niombe heka kumi za ardhi kwa ajili ya kufanya program za kisasa hadi leo sijapatiwa iyo ardhi na ipo wala haitumiki hadi Sasa nishasomesha wataalam wa kilimo zaidi ya 50 ndani ya jimbo wanavyeti hawana sehemu ya kufanyia kazi kama tutapewa iyo ardhi tutakombowa vitu vingi sana itakuwa mwiko kuagiza Nyanya vitunguu mbatata na mboga mboga mbali mbali.

Mh Pondeza alifika mbali kwa kusema kama serekali itaacha yote na kumuunga mkono basi ukosefu wa ajira utaounguwa kwa asilimia kubwa sana jambo litakalo ondowa tatizo la vijana kutumia madawa ya kulevya kwa sababu watakuwa na shuhuli za kufanya.

Ukisikia watu wanachoma mashamba ya miwa ujuwe kuna tatizo wamiliki wa kiwanda hawatakiwi wategemiwa wanayolima wao tu serekali ituwe mashamba watu walime miwa kwa wingi ili wakauze kiwandani lazima wanachi wafaidike na ardhi yao sio wizara ya ardhi kuzikumbatia matokeo yake wanaikosesha serekali mapato.

Mh Pondeza alisema mipango yote anayo iongelea inawezekana kutekeleza kama watapewa hayo maeneo aliyo yaorodhesha 

Akizungumzia changamoto ya ndani ya Jimbo lake amesema ni kambi ya Kipindupindu alisema awali wakati ikifunguliwa kambi hiyo wakaazi walikuwa sio wengi maaneo yale ila kwasasa kambi imezungukwa na makaazi ya watu nashauri serekali ihamishe kambi ya kipindupindu ndani ya chumbuni kama walivyo hamisha mnara wa kurushia matangazo ya ZBC ambao ulikuwa unathiri watu.

Kwasasa kuendelea kambi pale kunakosesha wananchi huma mbali mbali za kina mama na watoto kama chanjo kujifunguwa na huduma nyengine zote huwa zinasimama na wanachi wetu wanashindwa kwenda mbali kufata huduma izo matokeo yake takwimu za chanjo kwa watoto zinapunguwa kwa wananchi wa jimbo la Chumbuni.

Mh Amjadi alitoa wito kwa serekali Sasa wajipange kuondoa vyanzo vya maradhi ya Kipindupindu na wasisubiri kutibu Kipindupindu tena ilo jambo linawezekana kama serekali ilivyo maliza Malaria.

Kuna watu wanaishi maisha hatarishi sana nyumba hazina vyoo visima vinachimbwa karibu na mashimo ya vyoo wakaguzi wanakwenda wanaona ila hawazuii.

Mimi binafsi naamini bora kinga kuliko tiba 

Mh Ussi Salum Pondeza aliyasema hayo leo hii alipongea na waandishi wa habari mbali mbali kuhusiana na taasisi yake ya PONDEZA FOUNDATION inavyofanya kazi.

No comments:

Post a Comment