Tuesday, June 27, 2017

MUHTASARI WA RIPOTI YA KAMATI MAALUMU YA UCHUNGUZI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA DARUSO 2016/2017

Ndugu wanaDARUSO,

Mnamo tarehe 13.5.2017, Bunge liliadhimia kuundwa kwa kamati maalumu ikiwa ni matokeo ya Hoja nzito ya MH.Halima Juma(MB) juu ya matumizi mabovu ya fedha za DARUSO katka serikali ya mwaka 2016/2017.

Kamati iliongozwa na MUSSA YOHANA(M/kiti) na AWADHI AWADHI (katibu) pamoja na wajumbe wengine 7.

HADIDU ZA REJEA

Kamati iliongozwa na hadidu za rejea zifuatazo
1.Kuchunguza vyanzo vya mapato na uharali wake.
2.Kufanya mahojiano ya ana kwa ana na walengwa.
3.kutumia ripoti mbalimbali zilizopita ili kupata uwiano wa taarifa
4.kuchunguza matumizi ya wizara na ofisi mbalimbali za DARUSO.

MATOKEO YA RIPOTI
Kipengele hiki kimegawangika katika sehemu mbili.
A- upande wa mapato ya DARUSO
B- upande wa matumizi ya DARUSO

A. MAPATO YA DARUSO
Baadaya ya kupitia ripoti ya Waziri Mkuu NDUGU boniphance, aliyepita na kupitia vyanzo vya mapato, Kamati iligundua kua pato la vyumba vya stationary 6 alilo ainisha waziri Mkuu ilikua 2,230,000/= ambayo ni 17.4% badara ya milioni 5,700,000/=. Si hivyo tu, kiasi sahihi kilichotakiwa kuingia DARUSO ni Tsh 12,800,000/=.

Pia Bw. ERICK BONIVENTURE aliekua Waziri Wa sheria alijikusanyia Tsh 980,000/= kutoka Hall 1 stationary.Hazikupelekwa Benki hadi Leo.

ADA ZA UANACHAMA
Ripoti ya mach 2017 ya Waziri Mkuu wa DARUSO 2016/2017 inaoneshakua walipokea Tsh 97,095,000/=kama ada ya uanachama, haioneshi ni wanafunzi wangapi walidahiliwa. Ukweli kutoka Benki na Mhasibu Mkuu Wa chuo inaonesha pesa iliyoingia DARUSO ni Tsh 106,940,000/= sawa na wanafunzi 16,318 waliodahiliwa. Tofauti ya Tsh 9,845,000/=

WIZARA YA MIKOPO
Naibu Waziri Wa Mikopo bw. Erick Makupa alitumia zaidi ya Tsh 740,000/= ambazo zilitakiwa kulipwa kwa bw. Abdul Omar Nondo aliekua naibuwaziri Wa Mikopo kabla ya kujiuzuru pamoja na Ndugu Eliud Kasunzu aliekua Waziri Wa Mikopo kabla ya kutenguliwa katika nafasi yake.

MRADI WA SHATO
Mradi huu bado unautata katika mikataba yake pia kesi yake ipo mahakamani, hii inatupa utata kuujadili japo kuna harufu ya ubadhilifu mkubwa.

B. MATUMIZI YA DARUSO 2016/17
Makadilio ya bajeti ilikua Tsh 146,294,500/=

OFISI YA WAZIRI MKUU
Kamati iligundua ubadhilifu upande Wa manunuzi ya kamera, Ofisi ya Waziri Mkuu ilinunua Kamera aina ya CANON  yenye thamani ya Tsh 800,000/= badara ya 1,500,000/= iliyokua imeelekezwa.
*Wireless pot* upande Wa mabibo bado haikukamilika pia kuna ubadhilifu.
Pia bajeti ilitengwa kununua Visanduku vya maoni Tsh 400,000/= havikununuliwa.
Mbao za matangazo Tsh 250,000/= hazikununuliwa. Viti 25@10,000/= 250,000/= Havionekani.

WIZARA YA JINSIA NA MAKUNDI MAALUMU
Wazili alitengewe Tsh 300,000/= za harambee lakini hakufanya harambee na Fedha haikuludishwa DARUSO.

Ndugu wanaDARUSO,
Kamati ilikuja na mapendekezo yafuatayo;
1. Uongozi wachuo unapaswa kushilikishwa iliwaongeze nguvu katika madai ya DARUSO
2.Kuzuwia stahiki za wahusika Wa ubadhilifu huu, ikiwa ni pamoja na vyeti vyao
3. Nk.
Unaombwa kupitia ripoti hiyo ili upate taarifa kamili

MSIMAMO WA KAMATI
1. Itaandikwa barua kupitia kwa mshauri Wa wanafunzi kwenda kwa DVC, barua hii itasambazwa ofisi zote za UDSM ilikuzuwia stahiki za watu hawa.
2. Itaandikwa barua kuelekea TAASISI YA KUZUWIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA UDSM kwa ufuatiliaji zaidi. Pia kamati imeshakabidhi ripoti kwa Raisi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa UDSM. (CEOAC -UDSM).

Mussa Yohana (m/kiti kamati)
Awadhi Awadhi (Katibu kamati)
                   
                 @Jun. 24.2017

1 comment: