Monday, June 26, 2017

MBUNGE WA ILEMELA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

Katika  kuitumia siku yake ya mapumziko ya Sikukuu ya Eid El Fitr Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amefanya Ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa Jimboni kwake Ilemela chini ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya The Angeline Foundation katika kumaliza changamoto za muda mrefu zinazowakabili wananchi ikiwemo ukarabati wa majengo ya kituo cha Afya cha Buzuluga, Ujenzi wa Visima vya Maji kata ya Nyamhongolo, Mradi wa Ufatuaji Matofali kata ya Buswelu na Ufufuaji wa barabara zote zilizokuwa hazipitiki za kipindi cha Mkoloni sambamba na kuzungumza na wananchi vijiwe vya maeneo mbalimbali vya Jimbo

Akizungumza katika Ziara hiyo Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuendelea kuunga mkono Jitihada zote zinazochukuliwa katika kumaliza changamoto zote zinazokabili Jimbo hilo huku akiasa kulindwa, kuthaminiwa na kutunzwa kwa miradi yote inayotekelezwa

'... Lazima muwe na kamati ya kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi ya hii miradi mkizembea mkaiacha ikaharibika ni nyinyi ndio mtakao haribikiwa Mimi jukumu langu ni kuwabana wataalamu kukidhi viwango, ubora na pale zinapotokea changamoto maalumu ...' Alisema

Kwa upande wake Mhe Seleman Mabina M/kiti wa Mtaa wa  Kaguhwa Kata ya Nyamhongolo akiambatana na Diwani wa eneo hilo ulipo mradi Visima vya Maji mbali na kumpongeza na kumshukuru Mhe  Dkt. Angeline kwa Ujenzi wa Visima vya Maji kwa awamu ya kwanza na kumaliza kero waliyokuwa nayo wananchi wa eneo hilo ya kukosa Maji tangu kuanza kwa maisha ya wakazi hao  wamemuhakikishia kuitunza, kuilinda na kuithamini

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
25.06.2017

No comments:

Post a Comment