Marekani
imeendeleza ubabe wake wa kuzitungua ndege za kijeshi za Syria mara
baada ya kuitungua ndege nyingine isiyo na Rubani kusini mwa nchi hiyo.
Marekani
inadai kuwa ndege hiyo iliyotunguliwa ya Jeshi la Syria ilikuwa imebeba
silaha nzito na hatari kwa Jeshi la Marekani la ardhini hivyo imechukua
hatua hiyo kwaajili ya kujikinga na hatari ya kushambuliwa.
Hiki
ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani
kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine
isiyo na rubani mapema mwezi huu.
Katika
taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua
kiongozi wa cheo cha juu wa kundi la Islamic State Turki al-Binali,
wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment