Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo anawatangazia wananchi wote kwamba, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inatarajia kubaini na kuhakiki maeneo yote ya wazi pamoja na yaliyotumika awali kwa ajili ya utoaji huduma za maji kwa jamii yaani "PUBLIC WATER KIOSKS" Kata ya Sinza.
Kwa yeyote mwenye uhalali wa kuwepo kwenye maeneo hayo awasilishe vielelezo vyake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa uhakiki.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment