Friday, June 30, 2017

DC HOMERA APOKEA MADAWATI 300 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 30 TOKA KWA  MBUNGE WA TUNDURU KASKAZINI

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera, amepokea madawati 300 yenye thamani ya shilingi milioni thelathini toka kwa Mbunge wa Tunduru Kaskazini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Eng. Ramo Makani. Katika hafla iliyofanyika katika ofisi za maliasili wilayani Tunduru.

Katibu wa Mbunge wa Tunduru kaskazini, alimkabidhi mkuu wa wilaya ya Tunduru madawati hayo kwa niaba ya Mhe Eng. Ramo Makani, katika hafla fupi iliyo hudhuriwa na kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza Marando, wajumbe wa kamati ya siasa wilaya na makada mbalimbali wa CCM  Tunduru.

Mgawanyo wa madawadi hayo 300 yamegawiwa kwa shule za msingi 21 kama ifuatavyo.

1. Shule ya Msingi Jakika madawati-10
2. Shule ya Msingi Ruanda madawati  -10
3. Shule ya Msingi Pacha nne madawati-10
4.  Shule ya Msingi Mapambano madawati  - 15
5. Shule ya Msingi Kangomba madawati- 15
6. Shule ya Msingi Nakayaya madawati-15
7. Shule ya Msingi Mchangani madawati  -15
8. Shule ya Msingi Mataka madawati - 15
9. Shule ya Msingi Nangolombe madawati - 15
10. Shule ya Msingi Cheleweni madawati  -15
11. Shule ya Msingi Lelolelo madawati - 15
12. Shule ya Msingi Mwangaza madawati-15
13. Shule ya Msingi Mbugulaji madawati  -15
14. Shule ya Msingi Kalulu madawati - 15
15. Shule ya Msingi Mahau madawati - 15
16. Shule ya Msingi Jaribuni madawati -15
17. Shule ya Msingi Kindamba madawati  -15
18. Shule ya Msingi Kajima madawati - 15
19. Shule ya Msingi Mamiungo madawati  -15
20. Shule ya Msingi Ndenyende madawati  - 15
21. Shule ya Msingi Mnenje madawati - 15

Hadi sasa, Mhe. Ramo amekabidhi jumla ya madawati 882 katika awamu tatu, awamu ya kwanza madawati 45, awamu ya pili madawati 537 na awamu ya tatu madawati 300.

Akizungumza kwa niaba ya serikali Dc Homera, alisema kitakwimu kulikuwepo na upungufu wa madawati kwa shule za msingi ila madawati haya 300 yatamaliza tatizo hilo ila alimuomba mbunge wa Tunduru kaskazini aweze kusaidia shule ya sekondari Frank Weston madawati (viti na meza).

Aliendelea kwa kumpongeza Mhe. mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya na alimsihi aendele na moyo huo huo wa kuwakumbuka wananchi waliomchagua.

Aidha, Dc Homera alimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa halmashauri Ndg. Chiza Marando ili avipeleke katika shule zote 21 kabla ya shule kufunguliwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa halmashauri Ndg. Chiza Marando alimshukuru Dc Homera kwa kazi nzuri anayoifanya na pia alimpongeza mbunge kwa madawati Akinitoa.

No comments:

Post a Comment