Serikali
imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017 wenye
marekebisho ya sheria 15 ikiwamo Sheria ya Ushuru wa Bidhaa.
Kwa
mujibu wa marekebisho hayo, ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi
umeongezeka kutoka Sh 58 kwa lita hadi Sh 61 ikiwa ni sawa na ongezeko
la shilingi tatu.
Aidha,
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imepinga ongezeko hilo la shilingi
tatu kwenye vinywaji baridi ikisema hatua hiyo itazorotesha ukuaji wa
viwanda nchini.
Akiwasilisha
Muswada huo jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema
sheria hizo zinahusu masuala ya fedha, kodi, ushuru, tozo, na
mawasiliano ili kupunguza, kurekebisha, au kufuta viwango vya kodi,
ushuru, ada na tozo mbalimbali ili kuboresha ukusanyaji wa kodi.
Dk
Mpango alisema marekebisho hayo yamezingatia mkakati wa taifa wa kukuza
uchumi wa viwanda, na kwamba kiwango cha ushuru kwa baadhi ya bidhaa
zinazozalishwa nchini kimepunguzwa au kubakia ilivyo sasa.
Mengine
aliyozungumzia ni ongezeko la ushuru katika mafuta ya petroli, dizeli
na mafuta ya taa kwa Sh 40, Sheria ya Benki Kuu inayorekebishwa ili
kuweka sharti la ulazima kwa taasisi za serikali kufungua akaunti na
kuhifadhi mapato na fedha Benki Kuu.
Alisema
katika marekebisho hayo, pia ipo Sheria ya Posta na Mawasiliano ya
Kielektroniki ili kutoa wigo mpana kupanua wigo wa mauzo ya hisa za
asilimia 25 zitakazouzwa na kampuni ya mawasiliano kwenye soko la hisa
kwa kutoa fursa kwa Watanzania walio ndani na nje ya nchi, taasisi ya
Kitanzania, kampuni zinazomilikiwa kwa pamoja baina ya Watanzania na
raia wa nje, raia, kampuni na taasisi za nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki au raia na kampuni kutoka nchi nyingine.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti, Hawa Ghasia alipinga kuongezeka ushuru
kwa vinywaji baridi akisema hatua hiyo itapunguza uzalishaji.
Alitolea
mfano hatua ya serikali ya kutoongeza kodi kwenye bidhaa hiyo kwa miaka
mitatu iliyopita kuwa uzalishaji na uchumi uliongezeka na serikali
kupata kodi; huku akipendekeza tozo 14 zilizobakia katika shule na vyuo
binafsi zizidi kuondolewa ili wapunguzia gharama.
Mbunge
wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM), alisema muswada huo umejumuisha
asilimia 80 ya mapendekezo ya wabunge na kutaka asilimia 15 ya fedha
ambazo mashirikia ya umma hutakiwa kuchangia mfuko mkuu wa serikali,
zisitozwe kodi kwani mashirika ya umma yanalipa kodi mara mbili.
Mbunge
wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) alipendekeza kuongezwa tozo ya
asilimia sita hadi 12 kwenye mapato yatokanayo na michezo ya
kubahatisha, na asilimia nane hadi 20 kwenye zawadi na pia kuongeza tozo
ya leseni.
No comments:
Post a Comment