BALOZI wa Tanzania nchini Uingereza, Dk Asha-Rose Migiro (pichani)
amesema hakuna Mtanzania yeyote aliyeuawa wala kujeruhiwa katika
shambulio la bomu la Manchester, Arena nchini humo lililosababisha vifo
vya watu 22 na kujeruhi wengine 60. Dk Migiro aliliambia gazeti hili kwa
simu kuwa, mpaka jana mchana hakukuwa na taarifa za Mtanzania kufa au
kujeruhiwa katika shambulio hilo na kwamba ikiwa kutatokea taarifa,
wataujulisha umma wa Watanzania.
Awali, Polisi katika mji huo ilieleza kuwa uchunguzi unaendelea
kubaini kama tukio hilo la juzi lina uhusiano na ugaidi ingawa Waziri
Mkuu wa Uingereza, Theresa May
No comments:
Post a Comment