JESHI la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani limesema limeongeza
nguvu katika kusimamia sheria, kuboresha matumizi ya teknolojia na kutoa
elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya barabara ili kukabiliana na
ajali.
Limesema hatua hizo zimesaidia kupunguza matukio ya ajali nchini
Kamanda wa Kikosi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga
aliyasema Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari baada ya
kufunguliwa kwa Mkutano Maalumu wa Kanda kujadili na kutathmini
changamoto za usalama barabarani na jinsi ya kuzikabili.
“Mikakati tuliyo nayo sasa ni usimamizi wa sheria. Tumeendelea kuwa
wakali kwa wanaovunja sheria, matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa
sheria kwa kulipa faini kwa njia ya kielektroniki, kudhibiti mwendo
kasi na kutoa elimu kwa umma,” alisema.
Alisema, “Mwaka huu tutajipanua zaidi kwa kutumia teknolojia… Tuna
mpango wa kuweka kamera zitakazokuwa zikipiga picha katika maeneo
mbalimbali ili kuchukua hatua kudhibiti wanaovunja sheria.” “Tumelenga
kupunguza ajali kwa asilimia 50 ifikapo 2020,” alisema.

No comments:
Post a Comment