Mwenyekiti
Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa
nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika
mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni
Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai,
Dk. Feliciana Mmasi, Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti
wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), aliyemaliza muda wake
Dk.Elihuruma Mangawe (katikati), akiongoza kikao cha mkutano mkuu wa
chama hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TPHA, Fabian Magoma na kulia ni
Ofisa Utawala wa chama hicho, Erick Goodluck.
Mwenyekiti
Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo
(kulia) akiwaelekeza jambo wajumbe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi
uliompa nafasi hiyo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wa mkutano huo.
Usikivu katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Afya ya Jamii (TPHA) kimepata viongozi wapya ambapo kimemchagua Dk. Shaibu Mashombo kuwa Mwenyekiti.
Mashombo alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 na kumbwaga Feliciana Mmassy aliyepata kura 10 na kura moja ikiharibika.
Katika
nafasi ya Mhariri Mkuu Dk.Godfrey Swai aliibuka kidedea dhidi ya
Ndeniria Swai aliyepata kura 15 na kura tisa zilikataa ambapo katika
nafasi ya Katibu Mwenezi wagombea walikuwa wawili Elizabeth Nchimbi
aliyepata kura 15 na Ndeniria Swai ambaye aliibuka mshindi kwa kupata
kura 29 huku kukiwa hakuna kura iliyopotea.
Katika
nafasi ya Mtunza Fedha licha ya kuwepo na ushindani makali aliyeibuka
mshindi ni Mwanahamisi Hassan ambaye alipata kura kura 20 dhidi ya
mgombea mwenzake Violeth Shirima aliyepata kura 24.
Nafasi
ya Katibu wa Mipango ilikwenda kwa Dk. Mwanahamisi Hassan aliyepata
kura 38 dhidi ya Othman Shem aliyeambulia kura tano huku Feliciana Mmasi
na Dismas Vyagusa wakishinda nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.
No comments:
Post a Comment