Serikali inasema kuwa wale waliokamatwa walikata kufika kuhojiwa
Viongozi wa chama cha upinzani nchini Uturuki kinachowaunga mkono wakurdi cha HDP, wamekamatwa pamoja na wabunge wengine 9.
Selahattin
Demirtas na Figen Yuksekdag, wanalaumiwa kwa kueneza propaganda kwa
niaba ya wanamgambo wanaopigana vita na taifa la Uturuki.
Saa
chache baada ya bwana Demirtas kukamatwa eneo la Diyarbakir, mlipuko wa
bomu uliwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100.
Wanamgambo wamekuwa wakipigana vita kwa miaka mingi wakitaka kupata uhuru wa wakurdi.
Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari lililipuka baada ya viongozi hao kukamatwa
Uturuki imesalia chini ya amri ya hali ya hatari ambayo ilitangazwa baada ya jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwezi Julai.
Amri hiyo
inamruhusu Rais Recep Tayyip Erdogan na baraza lake la mawaziri
kutotegemea bunge wakati wa kupitishwa sheria mpya na kuvuta uhuru wa
watu.
Serikali
inasema kuwa wale waliokamatwa walikata kufika kuhojiwa, ambapo pia
waranti wa kukamatwa ulitolewa kwa wabunge wawili wa HDP ambao kwa sasa
wako chi za ng'ambo.BBC
No comments:
Post a Comment